Dem wa Facebook amtaka Pasta Ng'ang'a kuandamana na wahubiri wenzake katika maandamano

"Akumbushe pastor wakuje wote. Wavumilie teargas na bure wasipotujoin hatutoi fungu la kumi. Hatutatoa sadaka," alisema.

Muhtasari

•Dem wa Facebook aliapa kuingia mitaani Jumanne, Juni 25, kwa maandamano yaliyopangwa ya kupinga Mswada wa Fedha baada ya Mchungaji Ng'ang'a kutangaza atakuwepo.

•Mtayarishaji maudhui amemtaka Mchungaji Ng'ang'a kuwahamasisha wahubiri wengine kujiunga na maandamano hayo.

Dem wa FB
Dem wa FB
Image: Instagram

Dem wa Facebook ametoa wito kwa waundaji maudhui wa Kenya kujitokeza katika maandamano yaliopangwa Jumanne, Juni 25.

Akiongea katika mahojiano, mtayarishaji huyo wa maudhui alisema alifurahishwa na uamuzi wa Mchungaji Ng'ang'a kujitokeza barabarani katika maandamano dhidi ya mswada wa fedha 2024.

Alimtaka Ng'ang'a  kuwatambulisha na kuwahamasisha wahubiri wenzake kuhusu maandamano.

"Akumbushe pastor wakuje wote. Wavumilie teargas na bure wasipotujoin hatutoi fungu la kumi. Hatutatoa sadaka," alisema.

Dem wa Facebook pia aliwasihi waundaji wenzake wa maudhui kujiunga na maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha na sio kutazama tu mitandao ya kijamii.

"Tuamkie kwa barabara on Tuesday," alisema.

Hivi majuzi, Dem wa Facebook alishiriki maoni yake kuhusu Pendekezo la Mswada wa Fedha wa 2024.

 Akiongea katika mahojiano, alitoa maoni kwamba waundaji maudhui wanapaswa kusamehewa ushuru, akilaumu ukosefu wa kazi kutoka kwa serikali.

Mtayarishaji wa maudhui alisema, kwa kweli, serikali inapaswa kuanza kuwalipa waundaji wa maudhui badala ya kuwatoza ushuru.