Dorea Chege aeleza sababu za kutokuwa tayari kuzaa

"Nitapata mtoto nitakapohisi niko tayari.” Dorea Chege alisema.

Muhtasari

•Dorea Chege alisema kuwa kupata mtoto ni uamuzi wa hiari, na hatazaa tu kwa sababu watu wanamtaka, na kusisitiza kwamba atapata mtoto akiwa tayari.

•Dorea Chege na mpenzi wake,DJ Dibul , wamekuwa pamoja kwa muda lakini bado awajaliwa na mtoto.

Dorea Chege na Dj Dibul
Image: INSTAGRAM// DOREA CHEGE

Sosholaiti Mkenya na mwigizaji wa zamani wa Maria Dorea Chege ameeleza sababu inayomfanya hafikirii kupata watoto kwa sasa.

Dorea Chege alisema kuwa kupata mtoto ni uamuzi wa hiari, na hatazaa tu kwa sababu watu wanamtaka, na kusisitiza kwamba atapata mtoto akiwa tayari.

“Ni kwa sababu moja, hakuna mtu ananilazimisha kupata mtoto na mimi sipelekanangi na shinikizo la rika la watu."

"Nitapata mtoto nitakapohisi niko tayari.” Dorea Chege alisema.

Alieleza kwa kutoa mambo matatu ambayo yatamfanya apate mimba ambayo ni wakati anapokuwa na utulivu wa kimwili, kihisia, na kifedha.

"Lazima niwe na utulivu wa kifedha na utulivu wa kihisia kwa sababu mtoto huyo anahitaji mama wa aina hiyo," alisema.

Dorea Chege ambaye alipata jina lake la utani ‘Maggie’ alipokuwa mhusika kwenye kipindi cha Maria, kwa sasa amechumbiwa na Dj Dibul.

Wawili hao hawajawahi kukwepa kutangaza mapenzi yao hadharani.

Dorea Chege na mpenzi wake,DJ Dibul , wamekuwa pamoja kwa muda lakini bado awajaliwa na mtoto.