Mr Ibu kuzikwa Ijumaa miezi 3 baada ya kifo chake

Leo Alhamisi, Juni 27, kutakuwa na ibada ya Kikristo nyumbani kwa mwigizaji huyo eneo la Eziokwe Amuri, Nkanu Magharibi, Nigeria.

Muhtasari
  • "Nina huzuni sana kwamba siko na mume wangu hapa. Sina furaha hata kidogo baada ya juhudi na mateso yote tuliyopitia kuokoa maisha yake,” aliambia Vanguard
Marehemu Mr. Ibu.
Marehemu Mr. Ibu.
Image: REALMRIBU/INSTAGRAM

Mwigizaji na mchekeshaji wa Nigeria Mr Ibu atazikwa kesho Ijumaa Juni 28 miezi mitatu baada ya kifo chake.

Usiku wa heshima ulifanyika Jumatano katika jimbo la Enugu. Mke wa mwigizaji huyo wa Nollywood alikumbuka taabu alizopitia wakati akitafuta matibabu.

"Nina huzuni sana kwamba siko na mume wangu hapa. Sina furaha hata kidogo baada ya juhudi na mateso yote tuliyopitia kuokoa maisha yake,” aliambia Vanguard

Aliongeza;

“Sijui niseme nini! Nianzie wapi? Inasikitisha sana kuona mume wangu akilia kama mtoto mchanga nami, akisema "Oh darasa la kwanza ni mimi?" Nilikuwa namuangalia mume wangu akilia na kusaga meno. Nilikuwa naye hospitalini.

“Kuna wakati tulitaka kumsafirisha nje ya nchi kwa matibabu zaidi. Tulituma barua kwa hospitali mbili za India, Marekani na Ujerumani, lakini zote zilimkataa," alisema

Leo Alhamisi, Juni 27, kutakuwa na ibada ya Kikristo nyumbani kwa mwigizaji huyo eneo la Eziokwe Amuri, Nkanu Magharibi, Nigeria.

Siku ya Ijumaa, Juni 28, mwigizaji atazikwa.

Siku ya Jumapili, Juni 30, kutakuwa na sherehe ya shukrani kwa familia ya mwigizaji.

Jina halisi John Ikechukwu Okafor alizaliwa tarehe 17 Oktoba 1961 na kufariki tarehe 2 Machi 2024.