Eric Omondi alia kwa huzuni wakati wa ibada ya wafu kwa marehemu kakake, Fred Omondi

Katika moja ya video, Omondi anaonekana akilia kwa huzuni huku mpenziwe Lynne na mchekeshaji mwenza, Terence Creative wakimakribia na kumshikilia kumpa faraja.

Muhtasari

• Alikuwa ni mdogo wake Eric Omondi, na kaka wa pekee aliyekuwa amesalia kwa Eric baada ya kaka yao mwingine kufariki mwaka 2018.

 

ERIC OMONDI AKILIA KWA UCHUNGU WAKATI VWA IBADA YA WAFU YA KAKA YAKE
ERIC OMONDI AKILIA KWA UCHUNGU WAKATI VWA IBADA YA WAFU YA KAKA YAKE
Image: HULIO//MPASHO

Mchekeshaji aliyegeuka na kuwa mwanaharakati Eric Omondi na mpenziwe Lynne Njihia wamewasili katika makafani ya Chiromo asubuhi ya Ijumaa kwa ajili ya maandalizi ya safari ya mwisho na marehemu mdogo wake, Fred Omondi.

 Ibada ya wafu iliandaliwa katika makafani hayo ya Chiromo na picha na video zinamuonyesha Omondi akiwa katika hali ya huzuni.

Katika moja ya video, Omondi anaonekana akilia kwa huzuni huku mpenziwe Lynne na mchekeshaji mwenza, Terence Creative wakimakribia na kumshikilia kumpa faraja.

Omondi aliwasili asubuhi ya Ijumaa kutoka nyumbani kwao Sega, Siaya alikoenda wiki jana baada ya kukamilika kwa tamasha la mwisho kumuenzi Fred Omondi katika ukumbi wa Carnivore jijini Nairobi.

Tamasha hilo liliandaliwa na kundi la wachekeshaji humu nchini wakiongozwa na Churchill.

Baadae, mwili wa Fred Omondi utasafirishwa hadi Siaya na mazishi yake kufanyika Jumamosi ya Juni 29, kulingana na ratiba ya mipangilio ya mazishi iliyotolewa wiki jana.

Fred Omondi alifariki baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wiki mbili zilizopita.

Alikuwa ni mdogo wake Eric Omondi, na kaka wa pekee aliyekuwa amesalia kwa Eric baada ya kaka yao mwingine kufariki mwaka 2018.

Pole sana Eric!