logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Obinna aeleza sababu inayoweza kumfanya akose mazishi ya Fred Omondi siku ya Jumamosi

Fred Omondi alifariki baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wiki mbili zilizopita.

image
na Davis Ojiambo

Burudani28 June 2024 - 09:28

Muhtasari


  • •Fred Omondi alifariki baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wiki mbili zilizopita.
  • •Mazishi yaFred Omondi yatafanyika nyumbani kwao Siaya Jumamosi ya Juni 29.
  • •Obinna, hata hivyo, alisema hana uhakika kwamba atakosa kabisa mazishi ya Fred Omondi, lakini iwapo mmoja wa marafiki zake atapata chopa, basi anaweza kuwepo.

Mcheshi Oga Obinna ameeleza ni kwa nini hana uhakika kwamba atafanikiwa kufika katika mazishi ya Fred Omondi, licha ya kuwa ni wikendi.

Obinna, ambaye alikuwa akizungumza wakati wa onyesho lake la kila wiki pamoja na Dem Wa Facebook, alisema huenda akakosa kuhudhuria mazishi ya Fred Omondi kwa sababu siku hiyo atakuwa akiandamana barabarani, na kujenga ufahamu wa afya ya akili ya wanaume.

"Sitaweza kwenda kwa sababu nitakuwa nikifanya Men’s Mental Health Awareness Walk.

Nilianza haya kabla ya kifo cha Fred Omondi, na watu wengi wanahusika, na mimi ndiye mwanzilishi, kwa hivyo ni vigumu mimi kukosekana.

Lazima niwepo ili kuona maono hayo yakitimia.” Obinna alisema.

Obinna alithibitisha kuwa polisi wamewapa mwanga kuandamana barabarani na kuahidi kutoa usalama wanapotembea, akiwahimiza wanaume wote karibu na Nairobi kujitokeza katika bustani ya Uhuru park.

“Tutafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu bila malipo, kisha pia tutaongeleshwa kama mtaongeleshwa kama uko na stress bipolar and stress hiki ni kitu ambacho hutaki kukosa." Obinna alisema.

Obinna aliamua kuja na mpango huo kwa sababu, kwa mmoja, wanaume mara chache huzungumza, na kwa sababu takwimu za kimataifa zinaonyesha kuwa 75% ya watu wanaojiua ulimwenguni ni wanaume, anaamini kuwa mpango huu utawasaidia sana wanaume.

Obinna, hata hivyo, alisema hana uhakika kwamba atakosa kabisa mazishi ya Fred Omondi, lakini iwapo mmoja wa marafiki zake atapata chopa, basi anaweza kuwepo.

Fred Omondi alifariki baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wiki mbili zilizopita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved