“Nenda salama kakangu!” Ujumbe wa mwisho wa Eric kwa marehemu Fred Omondi

Katika klipu hiyo, Eric alionekana akifarijiwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye alimvuta karibu na kifua chake kama mwanawe na kumpapasa kwa kumfariji.

Muhtasari

• Baadae, Eric alipakia klipu kutoka kwa mazishi ya kaka yake na kutoa ujumbe wake wa mwisho baada ya Fred kuzikwa.

• “Pumzika kwa Amani Fred Omondi, nenda salama kaka yangu,” Eric Omondi aliandika.

ERIC OMONDI AMZIKA KAKA YAKE FRED OMONDI
ERIC OMONDI AMZIKA KAKA YAKE FRED OMONDI
Image: HISANI

Marehemu Fred Omondi alizikwa Jumamosi nyumbani kwao Sega, katika kaunti ya Siaya kwenye hafla ya mazishi ambayo ilivutia halaiki ya watu kutoka matabaka mbalimbali.

Katika hafla hiyo, wanasiasa kadhaa wakiongozwa na kinara wa ODM Raila Odinga na gavana wa jimbo hilo James Orengo walikusanyika kuomboleza na mchekeshaji aliyegeuka na kuwa mwanaharakati Eric Omondi.

Eric Omondi ambaye alionekana kulemewa na hisia alionekana akiwa ameshikiliwa na mpenzi wake Lynne Njihia wakati wote.

Baadae, Eric alipakia klipu kutoka kwa mazishi ya kaka yake na kutoa ujumbe wake wa mwisho baada ya Fred kuzikwa.

“Pumzika kwa Amani Fred Omondi, nenda salama kaka yangu,” Eric Omondi aliandika.

Katika klipu hiyo, Eric alionekana akifarijiwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye alimvuta karibu na kifua chake kama mwanawe na kumpapasa kwa kumfariji.

Mashabiki wa Eric walimhurumia kwa jinsi alivyokuwa mnyonge kwa kumpoteza kaka wa pekee aliyesalia naye baada ya kifo cha kaka mwingine miaka 6 iliyopita.

“Fred apumzike kwa Amani.!!! Neema na rambirambi KWAKO Eric na Familia.” Njugush alimwambia.

“Pole sana kaka … Kaka yetu aliyelala RIP” Patrick Salvado, mchekeshaji kutoka Uganga alisema.

‘pole sana Eric na familia! Pumzika vizuri Fred🙏🏾🙏🏾” msanii Nameless alisema.