Lucy Natasha aongoza maandamano ya amani Nairobi kuombea waathirika wa mandamano

“Tuko hapa kuomba, tuko hapa kuwakumbuka kujinyenyekeza mbele za Mungu na pia kuwakumbuka vijana wetu waliofariki. Kuna vijana wengi walioangamia katika maandamano,” aliongeza.

Muhtasari

• Katika maandamano hayo yaliyopewa jina ‘Heal Our Land’, Natasha aliongozana na mamia ya vijana waliokuwa wamevaa tsheti za rangi ya nyeupe kuashiria Amani.

Mchungaji wa kanisa la Empowerment Christian Church, ECC jijini Nairobi Lucy Natasha Jumapili aliandaa maandamano ya amani katikati wa jiji kuwaombea walioathirika katika maandamano ya ya kupinga mswada wa fedha wa 2024.

Katika maandamano hayo yaliyopewa jina ‘Heal Our Land’, Natasha aliongozana na mamia ya vijana waliokuwa wamevaa tsheti za rangi ya nyeupe kuashiria Amani.

Natasha alisema kwamba walilazimika kufanya hivyo kama njia moja ya kulaamika umwagikaji wa damu tena katika maandamano wiki hii.

“Leo tuko hapa kwa ‘Heal Our Land’ ni matembezi ya maombi kwa ajili ya vijana wetu na sababu iliyonifanya kuandaa maandamano haya ya Amani katika jiji hili ni kwa sababu kizazi chetu ni jukumu letu, na nilihisi lazima tufanye matembezi ya maombi ili kuomba,” Natasha alisema.

“Tuko hapa kuomba, tuko hapa kuwakumbuka kujinyenyekeza mbele za Mungu na pia kuwakumbuka vijana wetu waliofariki. Kuna vijana wengi walioangamia katika maandamano,” aliongeza.

 Mchungaji huyo pia alitoa wito kwa serikali kuwapa sikio vijana kwani wao ndio nguzo muhimu katika kuendelea kwa taifa.

“Tunaomba viongozi wetu kuwasikiliza vijana, wao ndio washikadau kwa hili taifa kuelekea maendeleo ya taifa hilo, Gen Z tunajivunia kwenu kwa kuonyesha mfano mzuri ila ningependa kuwashauri kuwa ni haki yenu ya kidemokrasia kutoa sauti zenu,” alishauri.