Davido agundua hesabu ya zawadi za pesa alizopewa harusini ni tofauti na pesa taslimu alizo nazo

Davido alienda kwenye sehemu ya maoni katika video hiyo na kutoa maoni hayo akisema kuwa pesa alizonyunyiziwa kwenye video za harusi hazilingani na kiasi walichopeleka nyumbani.

Muhtasari

โ€ข Wageni wengi walikuwa wamemzawadia mamilioni ya pesa ttaslimu kwa sarafu ya naira na fedha za kigeni

Image: Hisani

Mwimbaji wa Nigeria, Davido amezua vichekesho mitandaoni baada ya kufichua kule kinachoonekana kuwa wizi katika tukio kubwa la harusi yake wiki chache zilizopita.

Davido alichapisha katika kile kilionekana kama kulalamika kwa njia ya utani akisema kwamba amekuja kugundua kiasi cha pesa alizoona watu wakitoa kama zawadi kwa harusi yake hakiendani na hesabu kamili ya pesa alizokabidhiwa na waliosimamia shughuli nzima.

Kulingana na mkali huyo wa albamu ya Timeless,  huenda watu waliosimamia shughuli ya kupikea zawadi za harusi yake, haswa pesa, walificha baadhi yazo, kwani aliona zilikuwa nyingi tofauti na kiasi alichokabidhiwa

Aliandika;

"Video ya pesa zote nilizoona watu wakimwaga kwenye harusi yangu, hesabu yake haiendani na kiwango tulichobeba kwenda nyumbani."

Itakumbukwa kuwa Davido na mkewe, Chioma walifanya harusi yao tarehe 25 mwezi wa Juni na hafla hiyo ilihudhuriwa na mastaa wakubwa.

Wageni wengi walikuwa wamemzawadia mamilioni ya pesa ttaslimu kwa sarafu ya naira na fedha za kigeni.

Video ambayo inavuma iliyotumwa na mwanablogu Tunde Ednut inaonyesha wakati Davido alionekana aaktupiwa usoni burunguti la noti za dola wakati akitumbuiza kwenye harusi yake.

Davido alienda kwenye sehemu ya maoni katika video hiyo na kutoa maoni hayo akisema kuwa pesa alizonyunyiziwa kwenye video za harusi hazilingani na kiasi walichopeleka nyumbani