logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tom Daktari asimulia jinsi majambazi walivyoharibu gari lake

Shambulio hilo lilitokea alipokuwa akirejea nyumbani kutoka kwa maandamano wiki iliyopita kwenye gari lake

image
na Davis Ojiambo

Burudani03 July 2024 - 12:07

Muhtasari


  • •Kulingana na Tom Daktari, shambulio hilo lilitokea alipokuwa akirejea nyumbani kutoka kwa maandamano wiki iliyopita kwenye gari lake.
  • •Alieleza jinsi walivyomuibia mtu mbele ya macho yake wakati wa tukio hio.

Mcheshi wa Kenya Tom Daktari amesimulia tukio baya alilokuwa nalo na majambazi waliovunja vioo vya gari lake.

Kulingana na Tom Daktari, shambulio hilo lilitokea alipokuwa akirejea nyumbani kutoka kwa maandamano wiki iliyopita kwenye gari lake.

Alisema alikutana na majambazi hao akiwa njiani kurejea nyumbani—watu aliowataja kuwa ‘hawakusamehe’ kwa sababu alitazama jinsi walivyomwinua kijana mmoja na kumuibia mbele ya macho yake.

"Walinyonga mtu wakamuinua wakachukua simu, halafu naona 7 kati yao mbele yangu, na unaona siwezi tu kuendesha gari, kwa hivyo nikajiambia wacha nipunguze kasi, kisha ni kawaita," alisema.

Tom Daktari alidhani wanamfuata, akashusha vioo vya gari lake na kuamua kuzungumza nao huku akijaribu kuwauliza kwa upole iwapo walitaka kitu .

Alifikiri angeweza kuitumia fursa hio kuwaonyesha kwamba kweli hakuwa na tatizo nao na alichagua kuwa labda kwa kufanya hivyo wangemuacha.

"Ninawaambia, jamani, twendeni tukanunue maji huko au kitu yoyote. Lakini nilikua nataka kuwaambia hivyo, ndio wasinirushie mawe.” Tom Daktari alisema.

Mambo yote yaligeuka pale wale waliokuwa mbali walidhani kuwa anaibiwa na kuanza kurusha mawe ambayo yaliishia kuharibu gari lake.

Aliamua kuondoka baada ya kumuona mmoja akimsogelea, akitaka kuitoa iPhone yake mfukoni.

“Vile niliona anaendea iPhone yangu nikasema nikihesabu pesa ya hizi vioo haifikii iPhone yangu… nikasema simu ua viooo.

Vile niliona anaenda kuchukua simu nikakanyaga mafuta nikatoka, halafu baadaye nikaona mawe ndio inanifuata.” Tom Daktari alisema


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved