Jinsi Konshens alivyoonyesha upendo kwa Kenya akitumbuiza nchini Ujerumani

Konshens aliiona bendera ya Kenya na tukio hilo likamguza roho kiasi cha kuomba bendera hiyo aipeperushe hewani.

Muhtasari

•Konshens aliiona bendera ya Kenya na tukio hili likamguza roho kiasi cha kuomba bendera hiyo ili kuonyesha kusimama kwake na taifa la Kenya.

•Alichukua bendera hiyo na kuionyesha wakati alipokuwa akiimba, na hata kuomba mashabiki waiinamishe mbele na kuippeperusha jukwaani.

Konshens
Image: HISANI

Tamasha la Summerfestival 2024 lililofanyika Ujerumani lilikuwa la kukata shoka ambapo mwanamuziki wa dancehall Konshens alikuwa mmoja wa wasanii wakuu ambapo aliinua bendera ya Kenya alipokuwa akiimba muziki wake jukwaani.

Katika tamasha hilo, kulikuwa na mashabiki wengi  kupindukia ambapo Konshens aliiona bendera ya Kenya na tukio hili likamguza roho kiasi cha kuomba bendera hiyo ili kuonyesha kusimama kwake na taifa la Kenya.

Alipokuwa kwenye pilkapilka ya uimbaji, Konshens aliangalia mbele ya umati na kumtambua shabiki aliyeshikilia bendera ya Kenya akiwa kwenye mstari wa mbele kabisa kwenye tamasha hilo.

Aliuliza umati kama kuna mtu yeyote kutoka Kenya kisha akashirikiana nao kwa furaha na bashasha.

Alichukua bendera hiyo na kuionyesha wakati alipokuwa akiimba, na hata kuomba mashabiki waiinamishe mbele na kuipeperusha jukwaani. Baadaye, aliirudisha kwa mshabiki aliyekuwa ameishikilia.

Aidha, Konshens aliwashirikisha wanawake wakati wa tamasha hilo, akisisitiza kuhusu umuhimu wa wanawake huru na kujitambulisha kama msanii kutoka Kingston, Jamaica.

Vilevile aliitambua pia Uganda wakati wa burudani yake kwenye tamasha hilo.

Ni tamasha ambalo lilionyesha umoja wa tamaduni na burudani ya kimataifa, pamoja na heshima kwa mashabiki kutoka nchi mbalimbali.

Msanii huyo wa Dancehall wa Jamaika Konshens, hapo awali, alikuwa ameeleza kuunga mkono vuguvugu linaloongozwa na vijana akitaka Bunge kuukataa Mswada wa Fedha.