Krg the Don aeleza kwa nini alisapoti Mswada wa Fedha na Rais Ruto

"Nilikuwa naona tutateseka kwa mwaka mwingine, lakini baada ya hapo, tutakua tumelipa madeni mingi.” KRG alisema.

Muhtasari

•KRG ilisema aliunga mkono Mswada wa Fedha wa 2024 kwa sababu ulikuwa unaenda kuhakikisha kuwa nchi inalipa deni ambayo nchi inadaiwa na mataifa mengine.

•KRG pia alikiri kwamba alipokea jumbe na simu nyingi kutoka kwa umma lakini anashukuru kwamba hakutukanwa tofauti na wengi walivyofikiri angefanya.

KRG
KRG
Image: Instagram

Msanii wa Dancehall KRG The Don hatimaye ameeleza kwa nini alichagua kusimama na Rais William Ruto kuhusu Mswada wa Fedha wa 2024.

Akizungumza katika mahojiano, KRG ilieleza kuwa sababu ya yeye kuunga mkono Mswada wa Fedha wa 2024 ni kwa sababu Mswada huo ulikuwa unaenda kuhakikisha kuwa nchi inalipa deni ambayo nchi inadaiwa na mataifa mengine.

“Ndiyo maana mimi nilikuwa na support hii kwa sababu nilikua naona tutateseka kwa mwaka mwingine, lakini baada ya hapo, tutakua tumelipa madeni mingi.” KRG alisema.

Aliendelea kueleza zaidi kuwa hatetei kabisa watu kuandamana mitaani kwa sababu kuna masuala ya watu kupoteza maisha na uharibifu mwingi na hayo yanafanyika kwa jina la maandamano ya amani.

“Sikuona kama kulikuwa na haja ya kumwaga damu kwa sababu maisha ni kitu chenye huwezi recover hata na pesa ngapi.”

“Wachana na hao walikua wanasema walikuwa tayari kukufa mimi siwezi peleka mtoto wa mtu akufie kitu chochote kwa hii nchi wacha hata uongozi haikua imefika hiyo level ya watu kujipeleka kujitoa uhai hata kama maisha imekua ngumu aje.” KRG alisema.

Kuhusu suala la kukashifiwa na Wakenya, KRG pia alikiri kwamba alipokea jumbe na simu nyingi kutoka kwa umma lakini anashukuru kwamba hakutukanwa tofauti na wengi walivyofikiri angefanya.

“Salamu zenyu nazo nimezipokea sana na zilikuwa nzuri zingine lakini mimi ni mtu wa watu, wote wenye walinipigia wakisikia ni Bughaa walikua wanafurahia kabisa.

"Tunapiga story hiyo mambo walikuwa wanasema nitukanwe hakuna mtu alinitukana if that’s what maybe people expected kupokea simu nyingi tu.” KRG alisema

Baadaye Rais William Ruto alitupilia mbali mswada wa fedha wa mwaka 2024/25.

Rais alikiri kuwa wakenya wengi walionekana kuupinga mswada huo na licha ya kuwa serikali ilikuwa na mipango kupata pesa zaidi za maendeleo itabidi atafute njia mbadala.