logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilipta rafiki wa karibu! Brown Mauzo amlimbikizia sifa mpenziwe

Baadaye Kabinga aliweka picha hizo hizo kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram.

image

Burudani08 July 2024 - 11:06

Muhtasari


  • Wapenzi hao, ambao wamekuwa wakishiriki picha zao na kushiriki jumbe za mahaba, waliingia kwenye akaunti zao za Instagram kusherehekea hatua hiyo muhimu.
Brown Mauzo na mpenzi mpya.

Mwimbaji Brown Mauzo na mwanasosholaiti Kabinga Jr wametimiza mwaka mmoja tangu waanze uhusiano wao.

Wapenzi hao, ambao wamekuwa wakishiriki picha zao na kushiriki jumbe za mahaba, waliingia kwenye akaunti zao za Instagram kusherehekea hatua hiyo muhimu.

Akinukuu chini ya picha zao maridadi, Brown Mauzo aliandika,

"Happy anniversary my love@kabinga-jr ndani yako nilipata rafiki wa karibu msiri na mfuasi mwenye shukrani na aliyebarikiwa nina furaha kwa safari iliyo mbele yetu to many more my angel."

Baadaye Kabinga aliweka picha hizo hizo kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram.

Mauzo alimtambulisha Kabinga wiki kadhaa baada ya kutangaza kutengana na mwanasosholaiti Vera Sidika. 

"Ninakupenda kama vile sijawahi kukupenda maishani mwangu, kwa hivyo nipende kama vile haukuwahi kupenda maishani mwako," alisema mrembo huyo.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved