Sandra Dacha afichua ndoto ya mwanawe ni kukutana na mwanasoka Neymar siku moja

“Mapenzi yake kwa soka yalianza tangu zamani alipokuwa na umri wa mwaka mmoja na hapa tulipo sasa, Jeawel anafanya mazoezi na Ballers Of God Football Academy(BOG). Tafadhali nisaidie kumtakia bingwa wa siku zijazo mema,” Dacha alisema.

Sandra Dacha na mwanawe.
Sandra Dacha na mwanawe.
Image: Instagram

Mwigizaji Sandra Dacha ni mama mwenye fahari kushuhudia mwanawe akifikisha umri wa miaka 10.

Dacha alimsherehekea mwanawe wa kiume kwa picha kadhaa kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa amevalia mavazi ya kucheza kandanda pamoja na mpira mkononi.

Mwigizaji huyo alifichua kwamba mwanawe anapenda sana mchezo wa kandanda na kusema kila siku huwa anazunumzia jinsi anapenda kumtazana mchezaji kutoka Brazili, Neymar Jr akiwa uwanjani.

Dacha alisema kwamba ndoto ya mwanawe muda wote ni kukutana na mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona na PSG ambaye sasa anakipiga zake Saudi Arabia kwa klabu ya Al Hilal.

“UPENDO alionao mwanangu kwa mwanasoka huyu wa Brazil aitwaye NEYMAR ni nje ya dunia🤦🏿️🤣 anakunywa na kula kila siku akimtaja😆 na anachotamani ni kuonana naye tu siku fulani😇” Sandra Dacha alifichua.

Ili kumweka katika mkondo sahihi kutimiza ndoto yake, mwigizaji huyo anayejiita kwa jina la majazi la Biggest Machine alisema mwanawe huwa anafanya mazoezi katika academia moja ya soka.

“Mapenzi yake kwa soka yalianza tangu zamani alipokuwa na umri wa mwaka mmoja na hapa tulipo sasa, Jeawel anafanya mazoezi na Ballers Of God Football Academy(BOG). Tafadhali nisaidie kumtakia bingwa wa siku zijazo mema,” Dacha alisema.