Dem wa Facebook aeleza sababu ya kuwepo kwa kanisa nyumbani kwao

“Hiyo ni church, my dad, alijenga kwa boma. Sisi tunakuanga watu wa maombi , hapa kwetu kunakuanga na sheria za maombi.”

Muhtasari

•Akieleza sababu ya kuwa na kanisa nyumbani kwao alisema ni kwa kuwa kwao ni watu wa maombi na kwa sababu hiyo wana kanisa katika kiwanja chao.

•Pia Dem Wa Facebook alionyesha nyumba anayowajengea wazazi wake, nymba wa vyumba 3 vya kulala.

Dem wa Facebook

Mtayarishaji wa maudhui na mcheshi wa Kenya Dem Wa Facebook, kupitia chaneli yake ya YouTube, aliamua kuwafahamisha mashabiki wake kwa nini kuna kanisa nyumbani kwao.

Dem Wa Facebook ambaye aliyasema hayo alipokuwa akiwapa mashabiki wake ziara nyumbani kwao.

Pia alionyesha vyumba 3 vya kulala aliyokuwa akijegea wazazi wake.

Akieleza sababu ya kuwa na kanisa nyumbani kwao alisema ni kwa kuwa kwao ni watu wa maombi na kwa sababu hiyo wana kanisa katika kiwanja chao.

“Hiyo ni church, my dad, alijenga kwa boma. Sisi tunakuanga watu wa maombi 24-7, hapa kwetu kunakuanga na sheria za maombi.” Dem wa Facebook alisema huku akionyesha kanisa kwa mbali.

Anaendelea kueleza kuwa awali walikuwa wakitumia nyumba yao kama sehemu ya ibada hadi Watoto.

Hivyo Dem Wa Facebook na ndugu wengine walimshauri baba yao kufikiria kujenga nyumba tofauti ambayo inaweza kutumika.

“Tulisema hatuombei kwa nyumba, tunahitaji kuwa serious na maombi. Hiyo ni kanisa la familia yetu hata vile nimekuja lazima tuombe tusome verse, there’s power in prayer.” Dem wa facebook alisema.

Hata hivyo, Dem Wa Facebook alieleza kwamba alikuwa na wakati mgumu kujaribu kulala kwani hakuwa kwa dini kabisa kama vile wazazi wake walivyokuwa, lakini aliahidi kufuata nyayo za baba yake.