Watu wamhurumia Wema Sepetu kupokelewa airport na mbwa, wenzake wakipokelewa na watoto

“Nimejikuta machozi yananilengalenga aisee, Wema anatamani sana siku moja akitoka safari apokelewe namna hiyo na mtoto wake jamani. Mungu wa mbinguni akuguse tumbo lako kipenzi uitwe mama na wewe," mmoja alimuombea.

Muhtasari

• “Nimemkumbuka BabyGirl wangu...🐶🐶🐶 @vanillanunu. Ninahisi vizuri kurudi nyumbani ...” Wema Sepetu aliandika.

• Hali hii ilivutia baadhi ya mashabiki wake kumuonea huruma, ikizingatiwa kwamba mwigizaji huo kwa mara nyingi amekuwa akionesha nia ya kutapa kupata mtoto wake bila mafanikio.

WEMA SEPETU NA MBWA WAKE
WEMA SEPETU NA MBWA WAKE

Mashabiki na watumizi wa mtandao wa Instagram wameonesha hisia zao za huruma kwa mwigizaji wa muda mrefu wa filamu za Kiswahili kutoka Tanzania, Wema Sepetu baada ya kurejea nchini humo.

Sepetu alikuwa miongoni mwa waigizaji wa Tanzania waliokwenda ziara nchini Korea Kusini na walirejea Jumatatu.

Katika video za kurejea kwao, Wema Sepetu alionekana kufurahia kukaribishwa nyumbani na mbwa wake kwa jina Vanilla Nunu, ambaye anamtaja kama rafiki wa pekee katika maisha yake.

Wakati uo huo, wasafiri wenzake walionekana wakikimbiliwa na wanao kwa mbwembwe na kuwakabidhi maua, lakini kwa Wema, mbwa wake ndiye alijimkaribisha kwa kumkimbilia na kumrukia kwa furaha.

“Nimemkumbuka BabyGirl wangu...🐶🐶🐶 @vanillanunu. Ninahisi vizuri kurudi nyumbani ...” Wema Sepetu aliandika kwenye chapisho hilo la video ya makaribisho ya mbwa wake kwenye uwanja wa ndege.

Hali hii ilivutia baadhi ya mashabiki wake kumuonea huruma, ikizingatiwa kwamba mwigizaji huo kwa mara nyingi amekuwa akionesha nia ya kutapa kupata mtoto wake bila mafanikio.

Wema katika mahojiano ya awali alinukuliwa akisema kwamba muda mwingine anagutuka usiku wa manane na kujikuta anawaza tu sababu ya yeye kutokuwa na mtoto wake licha ya kujaribu dawa karibia zote.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya mashabiki wake;

“Mungu atujaaliye tusio na watoto tupate jamani 🥺🥺” @Dkt_irash.

“Dah😢 May our good God bless your womb 😍’ @Mama_G_Bakery_Moshi.

“Nimejikuta machozi yananilengalenga aisee, Wema anatamani sana siku moja akitoka safari apokelewe namna hiyo na mtoto wake jamani. Mungu wa mbinguni akuguse tumbo lako kipenzi uitwe mama na wewe. I heart u 😍😍😍” @womanunforgettable.

“Mimi ni mama wa watt watano mwanzo nilikua simuelewi wema kwann anampenda manunu wake lakini kwa sasa namuelewa mnooo ❤️endelea kumpenda mwaya kunawatu wanapewa upendo lakini awajui Kama wanapendwa Ukiondoka ndio wanajua upendo wako iogope kesho yako jilinde wewe mwenyewe” @sabrinadreadlocssalon.

Itazame hapa video hiyo;