Willy Paul atangaza mpango wa kuanza kuingia kwenye DM za warembo kuwapa kazi

Licha ya kuweka wazi kwamba ni suala la kazi tu litamfanya kuwafuata warembo wa sampuli anayoitaka kwenye DM, baadhi katika upande wa kutoa maoni walihisi ni ajenda nyingine ambayo analenga.

Muhtasari

• Msanii huyo anayezidi kutamba kwa albamu ya Beyond Gifted alisema kwamba atakuwa anaingia kwenye faragha za mabinti hao kuwapa kazi .

WILLY PAUL
WILLY PAUL
Image: INSTAGRAM

Msanii Willy Paul ambaye wiki chache zilizopita alidai kuhamisha Ujerumani ametangaza kuwa ana mpango wa kuwapa wasichana warembo kupita kiasi kazi kwenye DMs zao.

Pozee, kama anavyojiita alichapisha ujumbe huo kwenye Instastory yake akisema kwamba msichana yeyote ambaye ni mrembo kupindukia na anatumia mtandao wa Instagram, asishangae atakapomuona kwenye DM yake.

Msanii huyo anayezidi kutamba kwa albamu ya Beyond Gifted alisema kwamba atakuwa anaingia kwenye faragha za mabinti hao kuwapa kazi ambazo hata hivyo hakuweka wazi ni kazi za aina gani.

“Wewe ni mwanamke mrembo sana? Model type? Sawa, nitarajie kwenye DM yako mimi mwenyewe. Hivyo, ukiniona ninakuomba namba yako usishangae, niko na kazi kwako,” Pozee alichapisha.

Pozee amefunguka kuwa na mpango wa kuingia kwenye DM za warembo, miezi kadhaa baada ya baadhi ya watu kuvujisha mazungumzo kwenye DM ambayo yalidaiwa kuwa ya msanii huyo kwa warembo mbalimbali.

Licha ya kuweka wazi kwamba ni suala la kazi tu litamfanya kuwafuata warembo wa sampuli anayoitaka kwenye DM, baadhi katika upande wa kutoa maoni walihisi ni ajenda nyingine ambayo analenga.

Haya hapa ni baadhi ya maoni;

“Watu sii wajinga bwana 😂😂😂 one lege... anguka nayo 😂😂” @wangubest.

“Bora nisikuone kwa Dm ya Dem yangu ,😢nitaanguka nawewe😢” @boilingpoint_ke

“Wewee willy nakuona umeanz kujitetea apa kuna tea tunaanguka nayo BNN leta hio tea😂😂😂😂” @zuhuraswaleh59

“We tunakujua.... unataka kuanguka nao😂😂😂” @whoza.boy5