Mfanyabiashara Khalif Kairo amejibu madai yanayoenea kuwa anajihusisha na biashara wash wash baada ya shutuma za mwanamtandao kuhusu mali yake.
Biashara ya "Wash wash" ni neno ambayo Wakenya walibuni kumaanisha watu wanaopata pesa haramu lakini wanatumia biashara zao rasmi kusema kuwa pesa zao wakipata kupitia hapo.
Katika majibu yake, Kairo aliwataka Wakenya kuangalia picha zake za Facebook na kuona safari yake ya ukuaji kwani amekuwa akiuza magari kwa miaka 10.
“Ukiingia kwenye Facebook yangu na uangalie hadi ufikie picha zangu 2014, utaona safari yangu."
"kwa mambo haya lazima uamini utaratibu, watu wananiita wash wash kwa sababu ulianza. kuniona mwaka jana, lakini nimekuwa nikiuza magari, na huu ni mwaka wangu wa 10."alieleza.
Kairo aliongeza kuwa ameuza magari mengi kiasi kwamba hawezi kufuatilia idadi ya watu aliofanya nao biashara.
Alieleza jinsi anavyokutana na watu wanaomkumbusha kuhusu magari aliyowahi kuyauza siku za nyuma, lakini hana kumbukumbu.
“Mwamini Mungu, trust the process, jambo hili halihitaji pressure kwa hiyo mtu asikupee pressure."
"Fanya kazi yako tu, na usiruhusu mtu yeyote akushinikize. Na ujue kwamba Mungu anabariki," aliongeza.