Msanii Weezdom amelazwa katika hospitali ya Ladnan Pangani kaunti ya Nairobi,amefichua haya kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram..
Msanii huyo aliwafichuliwa mashabiki wake kwamba amekuwa mgonjwa kwa muda.
Aliwasihi sana wamuombee ili aweze kutoka hospitalini hapo akiwa hai na kuendelea na kazi zake za kawaida. Weezdom hata hivyo hakufichua ni nini hasa kilikuwa kinamsumbua.
“Hello fam, hope mko fiti. Kwangu siko fiti,nimekuwa mgonjwa kwa muda na nililazwa katika Hospitali ya Ladnan Panagani na bado niko hapo. Naomba maombi yako nitoke nikiwa mzima niendelee na hustle. Mungu awabariki nyote na asante kwa wenye wamenisupport, haijakuwa rahisi,” aliandika.
Katika chapisho tofauti, Weezdom alionyesha kukata tamaa, akitumai kuwa Mungu atamuinua kutoka kwa hali hiyo.
“Mungu nisaidie na sitawahi sahau au kusahau,” alisema.
Pia alimshukuru mpenzi wake ambaye amekuwa akipata muda wa kumtembelea hospitalini.
"Ninaweza kusema tu kwamba maisha ni ya thamani sana na kwamba wakati wa hali yako ya chini ni wakati unapojua watu wako. Na wewe ni mtu wangu, siku nzima unakaa kazini na bado unapita hospitali kuniona ninaendeleaje. Sijisikii vizuri lakini haujakata tamaa juu yangu. Huko nje kuna watu wenye nguvu sana, hawana hata mafua na wanaweza kukuondoa,” Weezdom alisema.