Mfanyabiashara wa Kenya Kennedy Rapudo alizungumzia hisia zake kama baba na mambo ambayo anatamani angefanya kwa njia tofauti.
Akizungumza katika mahojiano na jarida la Parents Africa, Rapudo alisema anatamani angempenda mwanamke mmoja, kufunga harusi na kupata watoto wao pamoja.
Rapudo ambaye ana watoto na wanawake watatu tofauti alisema kuwa maisha hayo hayawezekani katika ulimwengu wa sasa.
"Kuna mambo mengi sana ambayo ningetamani kuyafanya kwa njia tofauti kama baba, kwa mfano ningetamani kupata watoto na mwanamke mmoja tu, lakini tunaishi dunia tofauti..,” alisema.
Aliendelea kukiri changamoto ambazo akina baba ‘wengi’ wanakabiliana nazo katika jitihada zao za kudumisha uhusiano na watoto wao na kuwatia moyo wale walio katika hali kama hizo kudumu katika kupigania watoto wao.
Rapudo aidha alifichua jinsi alivyokutana na sosholaiti wa Kenya Amber Ray, ambaye sasa ni mama wa watoto wake.
"Alinikatia, kulikuwa mahali huko Thika road, ambapo watu walienda kuegesha magari, kutuliza, na kunywa."
" Kwa hivyo, nilienda pale nikiwa nimeegesha gari, na ndipo nikagundua kuwa kuna mwanamke ambaye alikuwa akinitazama kwa namna fulani iliyonifanya nitamani kumkaribia.”
Rapudo alieleza kuwa alichukua hatua ya kwanza ya kumsogelea na kuanza mazungumzo ya kumfahamu.
Walikutana tena, na mara wakaachana na wapenzi wao, wakaanza kuchumbiana.
“Mimi ndiye nilienda huko na kuongea naye, nikikiri kwamba alikuwa mrembo, na nilikuwa nimemuona kwenye mitandao ya kijamii.
Alikua na mtu na mimi nilikua na mtu, the moment alikua single hivi nikaingia mbio.” Kennedy Rapudo alisema.