Director Trevor ajizawadi Subaru Legacy akisherehekea siku ya kuzaliwa

Director Trevor alinunua Subaru Legacy B4 Ili kuadhimisha miaka 25 Yake ya Kuzaliwa.

Muhtasari

•Mwanzilishi wa Kenya Online Media Director Trevor alisherehekea miaka 25 ya kuzaliwa kwake kwa mtindo tofauti.

•Director Trevor alinunua Subaru Legacy B4 Ili kuadhimisha miaka 25 Yake ya Kuzaliwa.

Director Trevor na gari mpya aina ya subaru
Image: Instagram

Mtayarishaji wa maudhui na mwanzilishi wa Kenya Online Media Director Trevor alisherehekea siku ya kuzaliwa ya 25  kwa mtindo tofauti.

Director Trevor alinunua Subaru Legacy B4 Ili kuadhimisha miaka 25 Yake ya Kuzaliwa.

Trevor alifichua kwamba alikuwa amejiahidi gari jipya kwa siku yake ya kuzaliwa na alikuwa akiharakisha kulinunua kabla ya kufungwa kwa biashara.

"Leo ilikuwa siku yenye shughuli nyingi lakini nilijiahidi gari kwa ajili ya siku yangu ya kuzaliwa ya 25. Ninakimbia sasa kutafuta gari zuri kabla ya muuzaji kufunga."

Kisha alichapisha picha ya safari yake mpya na kujipongeza kwa kuwa mmiliki wa Subaru Legacy.

“Hongera kwangu kwa kuwa mmiliki wa legacy Subaru.”

Hivi majuzi, mtayarishaji wa maudhui na mwanzilishi huyo wa Kenya Online Media alifunguka kuhusu hali yake ya uhusiano na mwanamke bora kwake.

Mjasiriamali huyo kijana alikanusha madai ya kuwa kwenye uhusiano na mtu yeyote wiki chache tu baada ya kuachana na ex wake, Mungai Eve.

Hivi majuzi Trevor alikuwa amewaacha Wakenya wakishangaa kama kwamba amepata mpenzi mpya baada ya kushiriki picha za mwanamke ambaye alifunika uso wake.

Hata hivyo, alithibitisha kwamba mwanamke huyo alikuwa rafiki yake tu na kuweka wazi kuwa bado yuko sokoni, kinyume na walivyofikiri wengi.

"Alikuwa rafiki tu, na tulikuwa nje. Sasa hivi, ningetaka mwanamke ambaye anafanya kazi. Anapaswa kuonekana jinsi anavyoonekana. Unajua muonekano sio muhimu sana, tunaweza kununua sura. Hayo mambo mengine anapaswa kuwa nayo kwa hivyo asijali. Anaweza kuwa mkubwakuniliko au mdogo kuniliko," alisema