Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna alifichua kuwa pesa nyingi zaidi alizowahi kuchanga kwa harambee ni KSh 250,000.
“Pesa za juu zaidi ambazo nimewahi kuchanga ni KSh 250,000. Nilikuwa nimesave kutoka wakati wa uchaguzi kwa sababu ya hio harambee.”
“Mishahara yetu iko kwa umma nalipwa KSh 1 milioni. Zakayo anashuka na KSh 300,000.”
“Kuna watoto ninaowalipia karo kwa hivyo ninaondoa KSh 300,000 kutoka kwa mshahara wangu ili kuwalipia watoto karo. Sijui jinsi ya kuelezea. Binafsi, sina pesa," alisema.
Sifuna amefichua kuwa analipa karibu KSh 1 milioni kila mwaka kama karo ya shule.
Sifuna, kwenye Mic Cheque Podcast, alieleza uwazi kuhusu maisha yake ya faragha.
Seneta huyo alieleza kuwa amekuwa akiishi maisha duni kabla ya kuwa mwanasiasa.
Sifuna alisema kuwa hapendi kuonyesha au kushiriki familia yake kwenye mitandao ya kijamii.
Mshahara wa mwanasiasa huyo ulitiliwa shaka na kufichua kuwa anaishi sehemu moja upande wa Mombasa road.
“Mimi naishi side za Mombasa road kwa hiyo sitakiwi kutumia Expressway kwa sababu nikiitumia siwezi kuona vile hali ya barabara hiko kwa hiyo tunatumia Expressway na kutumia pesa za mwananchi, tunahitaji kujitafakari."
Seneta huyo alifichua kuwa mkewe anapata pesa zaidi kuliko yeye, na bibi wake huwa anamsaidia kila anapohitaji pesa taslimu.
"Mke wangu ni conservationist , anapesa nyingi kuliko mimi. Ako na doo mob huyo dem kunishinda. Saa hii bill ikinishinda namtumia SMS namshow babe niokoe ananitumia kitu."