Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna majuzi alijipata katika hali isiyotarajiwa baada ya nambari yake ya simu kufichuliwa kwenye mitandao ya kijamii.
Edwin Sifuna ni miongoni mwa viongozi ambao nambari zao za simu zilifichuliwa licha ya kutounga mkono Mswada wa Fedha wa 2024.
Akiongea wakati wa mahojiano katika Mic Cheque podcast, Edwin Sifuna alikiri kwamba kuna watu wabaya wanaojaribu kukashifu watu mashuhuri ambao wamejitahidi kujijenga.
Seneta wa Nairobi, ambaye alilazimishwa kushiriki kile msichana mmoja alimtumia, alisema kuwa huo ulikuwa ujumbe ambao hakuwahi kutarajia kupata.
“Wacha niwasomee moja, watu wameharibika bana, kuna dem anaitwa Ivy, mimi namwanika tu leo zile vitu watu wananiambia hapa kwa inbox. Hi, my name is Ivy Nimesikia, and you have been chewing on girls like nobody’s business."
"My only concern is where I can get the form so that I can sign up to volunteer.” Sifuna alisoma ujumbe huo.
Sifuna alichukua tukio hilo kwa mzaha, huku akiwashukuru kwa utani wale waliovujisha nambari yake.
“Wale walikua wanashare number yangu wanadhani wananiumiza mnanijenga mbaya… Ile kitu naeza ambia Ivy, line ni mrefu lakini inasonga.”