Mchungaji James Ng'ang'a amejibu shutuma za hivi karibuni za mwimbaji mkongwe wa nyimbo za Injili Faustine Munishi
Hivi majuzi Munishi alimkosoa Mchungaji Ng'ang'a kwa kusherehekea kutimuliwa kwa Mawaziri na Rais Ruto.
Munishi alimtaka Mchungaji Ng'ang'a kuwacha kujipongeza kwa maandamano yaliyoongozwa na Gen z.
Munishi alisema ni Mungu alitumia Gen Zs kupinga utawala mbaya na sio vile Ng'ang'a alisema ni majibu ya maombi yake.
Katika ujumbe wake Mchungaji Ng'ang'a alimwambia Munishi ashike njia yake na kusisitiza tofauti za mitindo yao.
“Hebu Munishi tuheshimiane, nimeona unasema mimi ni mkubwa kuliko wewe, mimi ni tajiri kuliko wewe, napiga gitaa huku unapiga kinanda, punguza ndevu zako."
“Munishi ungeweza kuvaa suti huku unanihutubia vyombo vya habari," Mchungaji Ng'ang'a alisema wakati wa ibada kanisani.
“Wewe ni mtanzania ukakimbilia kenya mimi niko kwetu najenga Kenya nenda ukajenge Tanzania hata kwa ngumi uniwezi.”
Baada ya mawaziri kutimuliwa Mchungaji Ng'ang'a alimshukuru Rais kwa jambo hilo.
“Kwa wale wasiojua kiingereza tafadhali zima TV yako, leo nataka niongee kwa Kiingereza kwa sababu rafiki yangu, waziri wa Barabara Kipchumba Murkomen ameenda nyumbani. Nenda, nilikuambia utaenda nyumbani.”
"Asante Mheshimiwa kwa kuwafuta kazi watu hawa." Alisema