logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hatimaye Mulamwah na Ruth K wametambulisha sura ya mwanao miezi 5 baada ya kuzaliwa

Kwa upande wake, Ruth K alimsherehekea mwanawe akimtaja kama mtu anayempa furaha muda wote.

image
na Davis Ojiambo

Burudani20 July 2024 - 13:14

Muhtasari


  • • Utambulisho huu ulikuja siku moja tu baada ya Ruth K kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
  • • Mulamwah katika ujumbe wake wa kumtakia Ruth K heri njema, alimtaja kama kitu cha maana zaidi kuwahi kutokea katika maisha yake.
MULAMWAH NA RUTH K

Hatimaye Mulamwah na mpenziwe Ruth K wamemtambulisha mwanao, Oyando Jr kwa mashabiki wao mitandaoni.

Wawili hao walitangaza mapema Ijumaa kwamba walikuwa wameratibu Jumamosi kuwa siku ya kipekee kwa mwanao ambaye alizaliwa mapema mwezi Februari mwaka huu.

Katika hafla hiyo ya kipekee ambayo wawili hao waliandaa na kuipeperusha moja kwa moja kwenye YouTube, walitambulisha sura ya mwanao na Mulamwah alimhongera mpenziwe Ruth K akisema kwamba waliunda kiumbe wa ajabu.

Mulamwah pia alimhongera mkewe Ruth K kwa kile alisema kwamba ni kumzalia mrithi wake na pia kuwashauri wanaume wenza kutokuwa na woga kuhusu kuanzisha familia.

“my main man ️ oyando jnr God literally said GOTHA TENA .. hey beb , tumeumba magic ... @atruthk thanks for the heir ️ , asante kwa kunipa familly , wanaume wapendwa usiogope kuanza tena,” Mulamwah aliandika.

Kwa upande wake, Ruth K alimsherehekea mwanawe akimtaja kama mtu anayempa furaha muda wote.

“Bingwa wetu mdogo🤗️ mshirika wangu anayecheza na mchekeshaji wangu😍unarahisisha nyumba yetu na kuijaza kwa upendo na furaha zaidi kila siku. Sehemu yangu ninayoipenda zaidi ni wakati wako wa kushikamana na papa.”

“Mama na baba wanakupenda sana na uendelee kuwa na afya njema na shangwe. Ulinzi wa Mungu na ukufunike daima️ Asante babe kwa kuwa siku zote kwa ajili ya mtoto wetu na kuweka muda wa kucheza na uhusiano daima ninajivunia wewe kwa kuwa baba na mume bora️familia yetu ya littu ndio kila kitu kwangu,” alisema.

Utambulisho huu ulikuja siku moja tu baada ya Ruth K kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Mulamwah katika ujumbe wake wa kumtakia Ruth K heri njema, alimtaja kama kitu cha maana zaidi kuwahi kutokea katika maisha yake.

“Furaha ya kuzaliwa malkia. wewe ni jambo bora kuwahi kutokea katika maisha yangu, umenirudisha hai. Nakupenda sana . asante kwa kila kitu , for the boy tooo . asante kwa support unayonipa kila wakati. Mungu akuinue siku zote , upate miaka mingi zaidi ya upendo , mafanikio , afya njema na mafanikio . ️ #HBD mama kalamz,” Mulamwah alimsherehekea mkewe.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved