KRG achagua biashara na kuacha muziki, “nitarudi kwa muziki nikishafikisha Sh132B kwa akaunti”

"Muziki nitarudi nikishafikisha dola bilioni moja [Ksh 131.5B] kwenye akaunti. Watoto wangu pia wanahitaji elimu ya kisasa hivyo inanibidi nipange maisha mapema,’ alisema.

Muhtasari

• Alisema kwamba kuna baishara zingine nyingi tu ambazo angependa kufanya na kujipatia faida si haba, huku akilenga kurejea kwenye muziki badae huko mbeleni.

KRG the DON.
KRG the DON.
Image: Screengrab

Mjasiriamali ambaye pia anajiita msanii tajiri zaidi Afrika Mashariki, KRG ametangaza kuchukua mapumziko kutoka kwa Sanaa ya muziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, KRG alitangaza kwamba baada ya tafakari ya muda, ameamua kuchukua mapumziko kutoka kwa Sanaa ili kuelekeza nguvu zake nyingi kwenye biashara zingine.

Alisema kwamba kuna baishara zingine nyingi tu ambazo angependa kufanya na kujipatia faida si haba, huku akilenga kurejea kwenye muziki badae huko mbeleni.

KRG ambaye amewahi nukuliwa mara si moja akidai kuwa utajiri wake ni zaidi ya bilioni 2 pesa za Kenya na kuwa ndiye msanii tajiri zaidi Afrika Mashariki alisema atarejea kwenye muziki akishaingiza Sh 131.5b kwenye akaunti yake.

“Ninachukua mapumziko kutoka kwa biashara ya Sanaa na burudani. Niko na kazi nyingi za kufanya, nahitaji muda wa kujikita zaidi katika biashara za maana mno kwa sasa. Muziki nitarudi nikishafikisha dola bilioni moja [Ksh 131.5B] kwenye akaunti. Watoto wangu pia wanahitaji elimu ya kisasa hivyo inanibidi nipange maisha mapema,’ alisema.

krg
krg

Awali, msanii huyo alikuwa amepapurana na Gen Z kwenye mtandao kuhusu msururu wa maandamano yao ya kuishinikiza serikali kuwajibikia matumizi ya ushuru wa Wakenya.

Kwa mujibu wa KRG, vijana hao wanastahili kutafuta njia mwafaka ya kumkabili rais ili kupata majibu yao kuliko kutumia fujo kwenye mandamano na matusi, akisema kwamba kwa itikadi hizo, taifa halitopata suluhu.

“Kuwaheshimu waliokuzidi umri ni jambo la maana wakati mwingine, hata kama wamekosea, tafuta njia nzuri ya kuwakabili, lakini matusi na vita havitaleta suluhu kwa matatizo yetu kama nchi,” KRG alishauri.