“Mimi ndiye mhubiri pekee ambaye anaombea watu wenye UKIMWI na wanapona!” - Kanyari

Akiwatoa wasiwasi waumini wake alisema kwamba yeye ndiye pasta pekee mwenye uwezo wa kukabili virusi vya UKIMWI na kuvitokomeza kabisa kutoka mwili wa mwathirika kupitia maombi tu!

Muhtasari

• “Mimi ndiye mhubiri pekee ambaye naombea watu UKIMWI na wanapona,” Kanyari alisema kwa sauti ya kijasiri.

• Hata hivyo, mchungaji huyo asiyeisha utata aliendelea akisema kwamba si kila mtu ambaye atamuombea atapona.

PASTOR VICTOR KANYARI
PASTOR VICTOR KANYARI
Image: HISANI

Mchungaji wa kanisa la Salvation Healing Minstry jijini Nairobi, Victor Kanyari ameibua madai mengine akisema kwamba yeye ndiye mchungaji pekee mwenye vibali vingi kutoka kwa Mungu.

Katika video moja inayopiga misele kwenye mitandao ya kijamii, Kanyari anaonekana akidai kwamba nchini Kenya, yeye ndiye mchungaji pekee mwenye kibali kutoka kwa Mungu cha kuponya virusi vya UKIMWI.

Kanyari akiwa kwenye mimbari ya kanisa lake, akiwatoa wasiwasi waumini wake akisema kwamba yeye ndiye pasta pekee mwenye uwezo wa kukabili virusi vya UKIMWI na kuvitokomeza kabisa kutoka mwili wa mwathirika kupitia maombi tu!

“Mimi ndiye mhubiri pekee ambaye naombea watu UKIMWI na wanapona,” Kanyari alisema kwa sauti ya kijasiri.

Hata hivyo, mchungaji huyo asiyeisha utata aliendelea akisema kwamba si kila mtu ambaye atamuombea atapona.

Kwa mujibu wake, kibali ambacho Mungu amempa ni kuwaombea watu wenye virusi vya UKIMWI lakini suala la ni nani atapona na ni nani hatapona baada ya kuombewa linasalia mikononi mwa Mungu pekee.

“…na si wote, ni yule mtu Mungu anataka apone!” aliongeza.

Hata hivyo, watu wengi walionekana kukinzana na kauli yake kwa dhana wazi kwamba virusi vya UKIMWI havijapata tiba kamili bali dawa zilizopo ni za kupunguza makali yake, wakisema kwamba hakuna kisa hata kimoja kimewahi ponywa kwa maombi, isipokuwa tu kwenye simulizi za Biblia enzi za Yesu na mitume.

“Wacha banghi mzee sasa,” mmoja alimwaambia.

“Apewe maziwa huyu, amechizi,” mwingine aliongeza.

“Hivi ndivyo ambavyo Mackenzi alianza,” mwingine alisema.