Mulamwah amevunja kimya chake kuhusu kile ambacho kimeonekana kuwa ni bifu linaloenezwa mitandaoni baina ya mashabiki wa babymamas wake.
Akizungumza kupitia kurasa za mitandao yake ya kijamii, mchekeshaji huyo aliomba mashabiki wa babymama wake Carrol Sonie na wale wa mpenzi wake wa sasa Ruth K kukoma kueneza chuki bali kuwaunga mkono wote katika utengenezaji maudhui mitandaoni.
“Mtandaoni kuna mambo mengi yanaendelea, kuna timu huku na kule, matusi, nini…mimi sina shida na hiyo stori, mimi nimepitia mbaya zaidi kuliko hiyo na mnanijua vizuri,” Mulamwah alianza.
“Nataka, these ladies manze wana’hustle sana. Ofcourse nikisema ‘these ladies’ mnajua nasema kina nani. Chenye mimi ningependa ni mwape support kila mmoja individually, wacha wajisukume. Adui wa mwanamke asikuwe mwanamke tena,” aliongeza.
Mulamwah alifchua kwamba Jumatano saa mbili usiku atakuwa live kwenye mitandao ya kijamii kujaribu kujibu maswali yote ambayo ameona watu wakiibua kaitka siku za hivi karibuni.
“Nitakuwa najibu maswali yenu yote hata Ruth K pia atakuwa anajibu maswali yenu yote. Mimi nataka kuona Amani mitandaoni, ndoto yangu ni kuona hawa watu wote ni wamoja. Nataka turudi mahali kwamba TikTok isikuwe ni mahali pa kutupiana matusi na kutengana, nataka iwe ni mahali pa kutengeneza chapaa na kubadilisha tulikotoka,” alisema.