Mchekeshaji Mulamwah ameamua kuweka wazi kuhusu maisha yake ya awali kabla ya kupata umaarufu kwenye Sanaa ya burudani kupitia ucheshi.
Mchekeshaji huyo ambaye amekuwa akijulikana kuwa na watoto wawili pekee kutoka kwa mama tofauti sasa amefichua kwamba Ana mtoto mwingine.
Kupitia Instagram, Mulamwah ambaye aliweka wazi kwamba alikuwa anaingia mbashara kwenye chaneli ya YouTube kujibu maswali yote alifichua hilo kwa mashabiki.
Akiambatanisha na picha, Mulamwah alisema kwamba mtoto huyo wa kike anaitwa Lisa na Ana umri wa miaka 7 anaelekea miaka 8.
Alisema kwamba mama yake mtoto huyo ambaye alikuwa mpenzi wake alifariki miaka kadhaa iliyopita na amekuwa akimlea mtoto hiyo kama single father kwa usaidizi wa wanafamilia.
"Binti kifunguamimba wangu Lisa. Ana umri wa miaka 7 anaelekea miaka 8. Tulimpoteza mama yake miaka iliyopita, lakini kila kitu kiko sawa," Mulamwah aliandika.
Alikiri kwamba ni siri ambayo amekuwa nayo bila mashabiki wake kujua.
Mchekeshaji huyo alisema kwamba hiyo ndio sababu aliamua kuingia mbashara mtandaoni kujibu maswali yote ambayo watu wangependa kujua.
"Kuna mengi mnayoyajua kunihusu, kuna mengine hamjui kunihusu. Leo nitawajibu nyinyi wote na kunyoosha maelezo kwa faida yetu sote," aliongeza.
Wengi wamekuwa wakijua kwamba ni baba kwa bintiye Carrol Sonie ambaye waliachana 2021 kisha baadae akachumbiana na Ruth K na kupata mtoto wa kiume mwaka jana.
Hivi majuzi, Mulamwah na Ruth K walifichua sura ya mwanao katika mitandao ya kijamii na jana alitoa wito mwa mashabiki kuwaunga mkono Sonie na Ruth K akisema wote ni wapambanaji.