Bonny Mwaitege aonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu taarifa za uongo za kifo chake

Alisema ametoa taarifa kwa maafisa wa eneo hilo ili kujua ni nani na jinsi habari hiyo ilianza.

Muhtasari
  • Mwaitege aliendelea kusema kuwa alikuwa na wasiwasi kwani mashabiki wake walibaki wakijiuliza ikiwa kweli yuko hai au la.
Mwanamuziki wa injili Bonny Mwaitege
Image: HISANI

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania Bonny Mwaitege ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu kuripotiwa kwa taarifa za uongo kuwa amefariki.

Hitmaker huyo wa 'Mke Mwema' alisikitishwa na watangazaji wa habari hizo kuthibitisha kuwa yuko hai na ni mzima. Akizungumza na umma katika video ya mtandao wa kijamii, mwimbaji huyo alisema;

"Nilitaka kujitokeza hadharani nizungumzie habari hizo za uwongo. Niliwahi 'kuuawa' kwenye mitandao ya kijamii mara kadhaa, lakini safari hii ilinishtua sana. Kwa kawaida huwa napuuza lakini kwa hili nilitaka. kuja kusafisha hewa."

Mwaitege aliendelea kusema kuwa alikuwa na wasiwasi kwani mashabiki wake walibaki wakijiuliza ikiwa kweli yuko hai au la.

"Kama unavyoniona niko hai na ni mzima. Si mgonjwa, sikupata ajali, ni habari za uongo tu,"

Aliendelea kuwataka watu watoe habari za kweli kwa wengine ili kupunguza mvutano "Sijajua ni nani aliyeanzisha hizi habari za uongo."

Alisema ametoa taarifa kwa maafisa wa eneo hilo ili kujua ni nani na jinsi habari hiyo ilianza.