Mwigizaji na mtayarishaji maudhui maarufu nchini Kenya Nyaboke Moraa, ameingia katika majonzi kufuatia kifo cha bintiye, Marrie Achieng.
Kifo cha Marrie kiliwekwa wazi na mwigizaji Sandra Dacha.
"Ni kwa masikitiko makubwa ninakutangazia kifo cha binti wa @nyabokemoraa. Maombi yako ndiyo anayohitaji kwa sasa🙏🏿 REST IN PEACE Marrie😭,” ilisoma chapisho kutoka kwa Sandra Dacha.
Chanzo cha kifo cha Marrie bado hakijawekwa wazi.
Kifo cha Achieng kinakuja zaidi ya mwezi mmoja baada ya mwigizaji Nyaboke kumpoteza kakake.
"Dakika moja tunafurahi na kufurahiya, dakika inayofuata tunapotea. Familia ya Nyariki imepigwa tena. Tumempoteza kaka yetu mkubwa. Tulisubiri uje kwa mkutano wetu lakini ulikosa safari yako ya ndege. Sasa tunaomboleza kifo chako cha ghafla.....hizi sasa hata ni gani hazieleweki???hatutapumua hii mwaka jameni katika familia yetu? Sigh, "alishiriki mnamo Juni 10, 2024
Mashabiki na watu mashuhuri ambao wameomboleza bintiye Nyaboke:
nanaowiti ;OmG! Nooooooooooooooo!! Nooooooo!!!!! 💔💔💔💔💔
nycewanjeri; Ooooh Nooooo 😭😭😭💔💔 Mungu ampe amani 🕊️
aggie_the_dance_queen ;Ooh no.Mungu ampe amani na familia yake🕊️🙏🏾
mwendemacharia; Oooo nooo..tukimuombea yeye na familia. Rambirambi zangu za dhati