Lupita Nyong’o asherehekea paka wake, Yoyo kufikisha umri wa miaka 3

Ikumbukwe Lupita aliasili paka huyo miezi 9 iliyopita, wiki moja baada ya kuweka wazi kwamba penzi lake na muigizaji mwenza, Selema Masekela lilikuwa limefika mwisho.

Muhtasari

• “Nenda Yoyo! Ni siku yako ya kuzaliwa! 💖🐈🎂 Tafadhali ungana nami katika kumtakia heri ya miaka 3 ya kuzaliwa!” Binti Nyong’o aliwarai mashabiki wake.

LUPITA NYONG'O NA PAKA WAKE.
LUPITA NYONG'O NA PAKA WAKE.
Image: INSTAGRAM

Muigizaji wa Kenya mwenye makazi yake nchini Mexico Lupita Nyong’o amesherehekea paka wake kwa kuhitimisha umri wa miaka 3.

Kupitia Instagram, binto huyo wa gavana wa Kisumu ambaye pia ni mshindi wa tuzo mahiri za Oscars mwaka 2014 alichapisha picha kadhaa akiwa amemuandalia paka wake sherehe ya kuadhimisha umri wa miaka mitatu.

“Nenda Yoyo! Ni siku yako ya kuzaliwa! 💖🐈🎂 Tafadhali ungana nami katika kumtakia heri ya miaka 3 ya kuzaliwa!” Binti Nyong’o aliwarai mashabiki wake.

Ikumbukwe Lupita aliasili paka huyo miezi 9 iliyopita, wiki moja baada ya kuweka wazi kwamba penzi lake na muigizaji mwenza, Selema Masekela lilikuwa limefika mwisho.

Lupita alitafuta faraja kwa paka huyo kama njia moja ya kumuondolea upweke, kwani bado hana mtoto.

“Namtambulisha mwenzangu mpya, Yoyo!Kihistoria nimekuwa nikiogopa paka, lakini maisha yangu yalipobadilishwa mara moja hivi karibuni, sauti kidogo ilininong'oneza kwamba ilikuwa wakati wa kukumbatia mabadiliko na uwezekano mpya. Kwa hiyo, rafiki mpendwa (shurani sana Palmer Hefferan!) alinishika mkono kupitia mchakato huo na kunipeleka kutembelea makao yangu ya kwanza ya wanyama,” alisema katika chapisho la kumkaribisha paka Yoyo kwenye nyumba yake.

Nyong’o alifichua kwamba kwa muda mrefu alikuwa anawaona kama wehu watu ambao walikuwa wamejaza picha za wanyama wa kuasili kwenye simu zao lakini baada ya kupigwa na upweke, aligundua maana na umuhimu wa kuwa na angalau kiumbe hai wa kukupa faraja.

“Nilimlea Yoyo kutoka Kituo cha Kuasili cha Marafiki Bora, na siku 3 ndani yake, nilijua singeweza kumchoka. Sikuwahi kuelewa watu ambao simu zao zilikuwa zimejaa picha na video za wanyama wao kipenzi - sasa mimi ni mmoja wa watu hao! Inaweza kuonekana kama nilimuokoa Yoyo, lakini kwa kweli, Yoyo ananiokoa,” Nyong’o aliongeza.