• Aliyasema haya wakati wa mazungumzo na Obinna kwenye chaneli yake ambapo aliulizwa ni vipi anaendelea kufaidi katika penzi hilo jipya.
• Kwa mujibu wa Trevor, mapenzi ambayo amelishwa kwa miezi 7 tu na Yvonne Kiki yanashinda yale ambapo aliwahi kupewa na mpenzi wa awali kwa miaka 5.
Mkurugenzi mkuu wa blogu ya Kenya Online Media, Director Trevor amefichua kwamba mapenzi anayopata katika penzi lake jipya hakuwahi kuyapata katika uhusiano wa awali kwa miaka 5.
Itakumbukwa Trevor alikuwa katika uhusiano na Mungai Eve kwa miaka 6 kabla ya kuachana na kumpenda Yvonne Kiki ambaye wamekaa pamoja kwa miezi 7 sasa.
Aliyasema haya wakati wa mazungumzo na Obinna kwenye chaneli yake ambapo aliulizwa ni vipi anaendelea kufaidi katika penzi hilo jipya.
Kwa mujibu wa Trevor, mapenzi ambayo amelishwa kwa miezi 7 tu na Yvonne Kiki yanashinda yale ambapo aliwahi kupewa na mpenzi wa awali kwa miaka 5.
“Mapenzi yenye huyu mrembo wa sasa ananipa sikuwahi kupewa kwa miaka 5. Ni miezi 7 tu lakini mrembo amenipiga na mapenzi. Ni mtu ako caring, ako tayari kunisapoti.”
“Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilipata huyu mrembo aliacha kazi yake ndio akuje kunisaidia kufanya kazi yangu. Kwa mara ya kwanza nimepata mtu ako willing ku’invest kwangu, kunisapoti. Hiyo miaka mingine nimekuwa mimi ndio nimekuwa nikifanyia watu vitu, sasa hivi yeye ndye yuko tayari kunifanyia,” Trevor aliongeza.
Akizungumzia jinsi walipatana na Yvonne Kiki, Trevor alisema kwamba mrembo huyo alikuwa mfanyikazi wa masoko kaitka kampuni moja iliyoko Ufaransa.
Alipotuma pendekezo la kutaka kufanya biashara nao, mrembo huyo ndiye aliyetumwa kama mwakilishi wa kampuni kwa mkutano huo ambao mwisho wa siku walikataa pendekezo la Trevor.
Hata hivyo, alisema kuwa licha ya pendekezo lake la kibiashara kukataliwa, pendekezo lake la mapenzi kwa mwakilishi wa kampuni hiyo lilikubaliwa na sasa wanahesabu miezi 7 na kuendelea katika mapenzi.