Nameless afichua picha ya mkewe Wahu ambayo ilikuwa ‘inamnyima usingizi’ akiwa chuo

“Hii picha ilikuwa inanimaliza nikiwa campo… i would look at it with a smile on my face before i go to sleep…sikuwa na amini huyu ni dame wangu," Nameless alifichua.

Muhtasari

• Siku nne zilizopita, Nameless alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo aliandikiwa ujumbe mtamu na mkewe akiibua kumbukumbu za jinsi mapenzi yao yaliota.

WAHU NA NAMELESS.
WAHU NA NAMELESS.
Image: INSTAGRAM

Siku chache baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kufikisha umri wa miaka 48, msanii Nameless amefichua picha adimu ya mkewe Wahu ambayo anadai ilimfanya kumpenda zaidi mama huyo wa mabinti 3.

Nameless alichapisha picha hiyo Instagram na kusema kwamba picha hiyo ya Wahu ni mahsusi kwake kwani ilikuwa inamkosha roho kiasi kwamba asingepata usingizi kila usiku kabla ya kuiangalia.

Msanii huyo mkongwe alieleza kwamba kila mara alipokuwa anaangalia picha hiyo, alikuwa haamini kabisa macho yake kwamba huyo ni mpenzi wake, akishukuru kuwa enzi hizo hakukuwa na mtandao wa Instagram kwani ungempa kiwewe watu kuona picha hiyo na pengine kumpokonya mpenzi.

“Hii picha ilikuwa inanimaliza nikiwa campo… i would look at it with a smile on my face before i go to sleep…sikuwa na amini huyu ni dame wangu ️… thank God there was no IG those days, nigekuwa insecure mbaiyaaa🤣🤣🤣… “ natamani ningekuwa mpasuko kwenye mavazi yako...” aliandika.

Siku nne zilizopita, Nameless alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo aliandikiwa ujumbe mtamu na mkewe akiibua kumbukumbu za jinsi mapenzi yao yaliota.

“HAPPY HAPPY BIRTHDAY to my beautiful husband, best friend, partner in crime na mengine mengi 😄😄😄. Kukutazama ukikua na kubadilika kutoka kwa kijana, hadi ….mwanamume ambaye ni mchanga moyoni 😄😄 (hatuzeeki! 😆) inafurahisha sana,” Wahu aliandika.

Wawili hao walifunga harusi mwezi Septemba mwaka 2004.