• Msanii huyo amekuwa katika mwanga wa lensi za waandishi wa habari za burudani katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mizozo isiyoisha katika maisha yake ya kimapenzi.
Msanii wa Mugithi na afisa wa polisi Samidoh amezua dhana isiyo maarufu kuhusu hulka ya wanaume kuwa wadanganyifu katika mapenzi.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Samidoh alichapisha kauli iliyoonekana kutetea tabia ya wanaume kuwadanganya wanawake wanaowapenda.
Akionekana kuwatetea wanaume na wakati uo huo kuwashauri wanawake katika mduara wa mapenzi, Samidoh alisema kuwa ni kawaida kwa mwanamume kumdanganya mwanamke anayempenda.
Kwa mujibu wa baba huyo wa watoto 5, hali ya mwanamume kuwa na mazoea ya kusema uongo kwa mwanamke anayempenda ni mbinu moja ya kuhakikisha kwamba analinda na kujali hisia za mhusika.
“Mwanaume anayekupenda atakudanganya kila wakati kwa sababu anajali hisia zako. Angependelea kukudanganya kuliko kuumiza hisia zako,” Samidoh alisema.
Msanii huyo amekuwa katika mwanga wa lensi za waandishi wa habari za burudani katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mizozo isiyoisha katika maisha yake ya kimapenzi.
Zogo lilianza mwaka 2021 alipokiri hadharani kwa kuchapisha ujumbe wa kuomba radhi kwa mkewe Edday Nderitu kwa kukiri kuchepuka na ‘kwa bahati mbaya’ kupata mtoto na Karen Nyamu.
Hata hivyo, miezi kadhaa baadae tena alijipata amerudi katika ubavu wa Karen Nyamu na kupata mtoto wa pili, jambo lililomuudhi Edday Nderitu kupelekea yeye kutangaza kujiondoa katika ndoa yake ya miaka 15 kwa kile alieleza kwamba hakuwa tayari kuwalea wanawe 3 katika ndoa yenye wake wengi kwa mume mmoja.
Kwa hiyo, Nderitu alifunga safari na wanawe wakaishia zao Marekani na kuapa kutompa Samidoh fursa ya kutangamana na wanawe, jambo ambalo hata hivyo lilikuja kuonekana kukiukwa hivi majuzi ambapo Samidoh alitembelea familia yake Marekani na kutangamana nao.