‘Iko kazi’: Thee Pluto atangaza kutafuta meneja, aorodhesha majukumu atakayotekeleza

Hivi majuzi, Thee Pluto alifichua kuwa alikuwa anajenga mradi wa nyumba za kuishi zaidi ya 18 katika eneo la Juja.

Muhtasari

• Kupitia insta story yake Jumapili usiku, Pluto alifichua kwamba katika maisha yake, hii ndio mara ya kwanza yeye kutafuta mtu wa kumsaidia katika kuendesha baadhi ya shughuli zake binafsi.

THEE PLUTO
THEE PLUTO
Image: INSTAGRAM

YouTuber Thee Pluto ametangaza kuwa anatafuta meneja wa kusimamia shughuli zake nyingi za kibinafsi.

Kupitia insta story yake Jumapili usiku, Pluto alifichua kwamba katika maisha yake, hii ndio mara ya kwanza yeye kutafuta mtu wa kumsaidia katika kuendesha baadhi ya shughuli zake binafsi.

Mkwasi huyo wa ukuzaji maudhui YouTube aliorodhesha majukumu 4 makuu ambaye meneja husika atakuwa anashughulikia akitoa wito kwa watu wanaoafiki matakwa yake yote kutuma maombi ya kazi kwake.

“Kwa mara ya kwanza ninamkubalia mtu kusimamia shughuli zangu,” Pluto alisema.

“Hivyo, ninatafuta meneja wa shughuli zangu binafsi, mtu ambaye anaelewa Sanaa ya burudani, mtu ambaye ni mbunifu na mwenye uelewa wa hali ya juu ambaye mawazo yake tunaweza kuyategemea, mtu ambaye anaelewa Sanaa yangu, jinsi mimi hufanya mambo yangu na anahisi kwamba bado kuna nafasi kubwa ya maboresho na ambaye kwa kweli ana mawazo mapya,” Pluto aliorodhesha.

“Mtu ambaye ana uelewa na ujuzi kuhusu masuala ya kifedha, na anaweza kuandika ripoti za kifedha, kutayarisha akaunti za fedha na kutoa ushauri wa kifedha na majukumu mengine kwenye mkondo huo,” baba huyo wa binti mmoja aliongeza.

Kijana huyo amekuwa akionyesha utajiri wake katika mitandao ya kijamii, ambao amewaaminisha wengi kuwa ameupata kutokana na juhudi zake katika kutengeneza maudhui kupitia jukwaa la YouTube.

Hivi majuzi, Thee Pluto alifichua kuwa alikuwa anajenga mradi wa nyumba za kuishi zaidi ya 18 katika eneo la Juja.