Brown Mauzo amnunulia mpenziwe Kabnga Jr chupi za kutumia mwaka mzima

Zawadi hizi zinakuja siku chache tu baada ya Mauzo kudokeza kwamba penzi la Kabinga limemkolea mpaka kumrejeshea mshawasha wa kutaka kurudi kwenye ndoa rasmi tena

Muhtasari

• Msanii huyo alimpa mpenziwe kifurushi hicho ambacho baada ya kukifungua, Kabinga alipigwa na butwaa kufahamu kilichokuwa ndani.

BROWN MAUZO NA MPENZIWE
BROWN MAUZO NA MPENZIWE
Image: FACEBOOK

Brown Mauzo amemshangaza mpenziwe Kabinga Jr kwa zawadi adimu bila kutarajia.

Mauzo alichapisha video akiwa amebeba shada la maua na kifurushi kukubwa kilichopambwa vizuri na kumshtukizia Kabinga nyumbani.

Msanii huyo alimpa mpenziwe kifurushi hicho ambacho baada ya kukifungua, Kabinga alipigwa na butwaa kufahamu kilichokuwa ndani.

“Zawadi ndogo, maua ya upendo, divai mahali petu, sio lazima gharama ya pesa, inahitaji tu kumshtukizia. Anastahili zaidi ya hii ...Ukuu wake wa kifalme. Ilibidi nimshtue tu,” Brown Mauzo aliandika.

Alionyesha kwenye kamera makumi ya nguo za ndani ambazo Mauzo alimnunulia kama zawadi, akifichua kwamba nguo hizo zitampa huduma kwa mwaka mzima na kumshukuru Mauzo kwa zawadi hiyo.

“Ahsante kwa maua mpenzi wangu, nimeyapenda. Na chupi ni za matumizi ya mwaka mzima, Brown Mauzo nimeokoa mfuko wako pakubwa sasa,” aliandika kwenye video hiyo Kabinga Jr.

 Zawadi hizi zinakuja siku chache tu baada ya Mauzo kudokeza kwamba penzi la Kabinga limemkolea mpaka kumrejeshea mshawasha wa kutaka kurudi kwenye ndoa rasmi tena.

Msanii huyo ambaye alitengana na Brown Mauzo mwaka jana aliweka wazi kwamba hivi karibuni atafikiria kufunga ndoa na Kabinga na kumfanya kuwa mke wake rasmi.

"Huyu malaika ananipa mshawasha wa kutaka kuoa tena. Ninathibitisha. Hebu na tuwe na hafla kubwa hivi karibuni. Maombi yenu ndio tunahitaji," baba wa watoto wawili na Vera Sidika alifichua.

Mauzo na Kabinga wamekuwa wakichumbiana kwa takribani miezi 11 sasa, kwani waliweka wazi uchumba wao siku chache tu baada ya kutangaza kuvunjika kwa ndoa yake na Vera Sidika mwishoni mwa Agosti mwaka jana.