•Justina anamnunulia mwanawe gari kama zawadi yake kwa kufikisha umri wa miaka 14.
•Justina Syokau ni msanii wa injili ambaye anajulikana na wimbo wake wa "Twendi Twendi"
•Ni mama ya mtoto mmoja.
Msanii wa injili Justina Syokau amemnunulia mwanawe gari jipya baada ya kumpa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa alipofika umri wa miaka 14.
Justina alishiriki video kwenye Tiktok akionyesha jinsi alivyomshangaza mwanae, hali iliyoacha mashabiki wake na maoni tofauti. Katika video hiyo, Justina alikuwa amefunga mwanawe macho wakati alikuwa akimpeleka nje ya hoteli kumuonyesha gari nyekundu ambalo alikuwa amemnunulia.
Mara tu alipomruhusu kuona,mwanawe alifungua kinywa chake kwa mshtuko na kuuliza mama yake kama hilo lilikuwa gari ambalo mtu amempea. Justina alimwambia kwamba gari hilo lilikuwa lake, na mwanawe akamuuliza "umetoa pesa wapi?". Mama yake alicheka na kumjibu "Nakupenda sana, nataka ujue kuwa nakupenda. Hii ni gari yako. Hii ni zawadi yako ya kuzaliwa, ya mwaka wako wa 14 sawa mtoto wangu?. Nakupenda sana...Hii gari nimekupatia......" Aliweza pia kumtambulisha dereva ambaye atakuwa anapeleka mwanawe popote atataka kuenda.
Syokau alisema sherehe hiyo ilikuwa ya kumshukuru Mungu kwa kumfikisha mahali alipo.
Justina Syokau anajulikana kwa nyimbo:"Twendi Twendi", "Twendi Twendi Wani" na zingine nyingi. Yeye ni mama wa kijana mmoja kwa jina Nixon Musyoka ambaye amefikisha umri wa miaka 14 mwezi huu.