•Mp Salasya aonyesha mchoro wa nyumba ambayo amewazia kujenga kijijini akisema kuwa hawezi kuwa na nyumba nzuri Mjini kuliko kijijini alikozaliwa mtaa wa Kisumundogo.Ni jambo ambalo wafuasi wako wamelikubali na kumpongeza kwa bidii yake kijendeleza.
Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Selasya ambaye huvutia wafuasi wengi kutokana na ucheshi wake ,sasa ameonyesha mchoro wa jumba ambalo amewazia kujenga kijijini maoneo ya Kisumundogo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook PK amesema kuwa maono yake ni kujenga jumba ambalo ametoa mchoro wake pale nyumbani ambako ndiko chimbuko lake.
"Nyumbani ni kwema kila wakati,na pendelea kujenga nyumba kijijini pale Kisumundogo Mumias East lakini si Nairobi.Wakati unajenga nyumba katika kijiji,'ancestors' wanafurahia,siwezi kuwa na nyumba nzuri Nairobi kushinda kijijini,na hili ndilo litakuwa jumba pale Mumias East,Mungu akijaalia", alisema.
Ikumbukwe ni siku chache baada ya PK kutangaza kuwa anatafuta mwanadada ambaye atakuwa akimpikia licha yake kuchoka kupikiwa na wanaume ugali kwa sukuma kwa mujibu wa alichosema,"Nimechoka kupikiwa ugali na sukuma kila siku na wanaume wezangu " .
Kutokana na posti hiyo baadhi ya wafuasi wake walionekana kufurahishwa na wazo hilo huku nwengi wafanya mzaha na kusema kuwa ni jirani yake atakuwa akimtembelea "eeeeeiii nitakuwa nakutembelea kila wikendi kukuletea matunda na mboga za majani,harakisha" mfuasi alisema,Vile vile vijana wenzake hawakuachwa nyuma huku wakisema "eeei hapa itabidi vijana wewe nana room ya mzinga hapo rooftop"...alisema kwa utani .