Pasta aliyemuonya Osimhen dhidi ya kuenda Chelsea amshauri kuenda Arsenal

Mchungaji huyo alisisitiza kwamba nyota ya Osimhen haitang’aa katika klabu ya Chelsea.

Muhtasari

• “Osimhen hatang’aa katika klabu ya Chelsea. Kama ataenda Chelsea hawezi furahia. Acha aende Arsenal,” Pasta huyo alishauri.

VICTOR OSIMHEN
VICTOR OSIMHEN
Image: FACEBOOK

Mchungaji wa Nigeria aliyetoa onyo kali dhidi ya mchezaji wa kimataifa wa Nigeria na klabu ya Italia ya Napoli, Victor Osimhen dhidi ya kujiunga na klabu ya Chelsea ametoa onyo lingine tena.

Pasta Primate Ayodele safari hii kando na kumuonya Osimhen dhidi ya Chelsea, pia amempa ushauri kijana huyo kujiunga na Arsenal badala yake.

Mchungaji huyo alisisitiza kwamba nyota ya Osimhen haitang’aa katika klabu ya Chelsea.

“Osimhen hatang’aa katika klabu ya Chelsea. Kama ataenda Chelsea hawezi furahia. Acha aende Arsenal,” Pasta huyo alishauri.

Mchungaji huyo akizungumzia uwezekano wa uhamisho wa kwenda Chelsea kwenye video iliyowekwa kwenye X, mchungaji Primate Ayodele alifichua kwamba uhamisho huo unaweza kuwa usio na manufaa kwa Osimhen.

Kwa mujibu wa mtu huyo anayejiita Nabii anayeona na kutabiri mambo ya kiroho, Osimhen kujiunga Chelsea haitakuwa tu mkosi kwake mwenyewe na taaluma yake ya soka bali pia itakuwa ni mkosi mkubwa kwa timu ya taifa lake.

“La kwanza ni onyo kwa Osimhen: ‘Ngoja nikuambie kwa haraka kwamba hupaswi kabisa kuhamia Chelsea kwa sababu ukifanya hivyo, hutafaulu na utakuwa mwisho wa taaluma yako’” alionya.

Mchezaji huyo bora wa Afrika amekuwa akiwindwa na klabu za Paris Saint-Germain na Chelsea.

Walakini, vilabu vyote viwili vinasemekana kusita kukubali bei inayodaiwa ya Napoli ya euro milioni 130 kwa mchezaji huyo wa miaka 25, ambaye bado yuko chini ya kandarasi hadi 2026.

Habari za sasa zinaonyesha kuwa kuna uwezekano wa kuwa na mazungumzo zaidi kati ya Chelsea na Napoli katika siku za usoni.