Brown Mauzo aanzisha kampeni ya kuwazawadi kina dada chupi

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Brown Mauzo alichapisha picha ya rundo la chupi na kufuatisha na ujumbe kwamba angependa kuwapa kama zawadi kina dada kadhaa nguo hizo za kujisitiri.

Muhtasari

• “Kesho nitawapa kina dada chupi za kupendeza, weka maelezo ya maeneo yenu ya kupokea kwa ajili ya hizi zawadi,” Mauzo aliandika.

Image: INSTAGRAM

Msanii Brown Mauzo ametangaza kuanzisha mchakato wa kuwatunuku kina dada nguo za ndani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Brown Mauzo alichapisha picha ya rundo la chupi na kufuatisha na ujumbe kwamba angependa kuwapa kama zawadi kina dada kadhaa nguo hizo za kujisitiri.

Mauzo aliwataka kina dada wenye haja kuweka namba zao na maeneo walipo kwa ajili ya kurahisisha mchakato wa kutumiwa zawadi hizo.

“Kesho nitawapa kina dada chupi za kupendeza, weka maelezo ya maeneo yenu ya kupokea kwa ajili ya hizi zawadi,” Mauzo aliandika.

brown mauzo
brown mauzo

Tangazo hili linakuja wiki moja tu baada ya Brown Mauzo kumnunulia mpenzi wake, Kabinga Jr nguo za ndani nyingi ambazo Kabinga alifichua kuwa zina uwezo wa kumhudumia kwa hadi mwaka mzima bila kurudi sokoni.

Msanii huyo alimpa mpenziwe kifurushi hicho ambacho baada ya kukifungua, Kabinga alipigwa na butwaa kufahamu kilichokuwa ndani.

“Zawadi ndogo, maua ya upendo, divai mahali petu, sio lazima gharama ya pesa, inahitaji tu kumshtukizia. Anastahili zaidi ya hii ...Ukuu wake wa kifalme. Ilibidi nimshtue tu,” Brown Mauzo aliandika.

Alionyesha kwenye kamera makumi ya nguo za ndani ambazo Mauzo alimnunulia kama zawadi, akifichua kwamba nguo hizo zitampa huduma kwa mwaka mzima na kumshukuru Mauzo kwa zawadi hiyo.

“Ahsante kwa maua mpenzi wangu, nimeyapenda. Na chupi ni za matumizi ya mwaka mzima, Brown Mauzo nimeokoa mfuko wako pakubwa sasa,” aliandika kwenye video hiyo Kabinga Jr.