CEO wa Bonfire Adventures Simon Kabu amfadhili Bradley kwenda Mombasa

"uende Mombasa upande ndege...uende kwa swimming pool atleast ufurahie" Simon Kabu

Muhtasari

• Kwenye video ambayo Kabu aliweka kwenye ukurasa wake ya Facebook, alionekana akimkaribisha Bradley kwa furaha na hata kupanda juu ya kiti ili aweze kutoshana na yeye.


Bradley Mtall
Bradley Mtall
Image: Bradley Mtall//Facebook

Baada ya dhiki faraja, Bradley Mtall amekuwa akivuma katika mitandao ya kijamii si kwa urefu wake tu bali pia kwa mafanikio yake ambazo ameweza kupata katika wiki hizi chache zimepita.

Jumanne jioni Mkurugenzi Mtendaji wa Bonfire Adventures, Simon Kabu alimpatia Bradley  ziara ya siku tatu kuzuru Mombasa.

Kwenye mtandao wa kijamii (Facebook) Kabu aliandika " Bradley aka Gen Z Goliath.Ni masaa yake na BONFIRE ADVENTURES AND EVENTS...a 3 day Coast Holiday imeiva soonest plus some token and mentorship for him to do something better." 

Aliongeza "Uende Mombasa upande ndege....apande ndege aende Mombasa...uende kwa swimming pool atleast ufurahie.....then after that atleast kuna katoken nitakupatia ili uweze kujijenga"

Kabu alimwambia Bradley yakwamba ikiwa atataka mawaidha yoyote anaweza kumpigia ili amshauri. Aliwambia kuwa umaarufu unakuja na autumie vizuri, pia alimshauri awe akiweka ile kitu kidogo anapata kwenye akaunti yake ya benki ili aweze kuitumia miaka ijayo.

Kwenye video ambayo Kabu aliweka kwenye ukurasa wake ya Facebook, alionekana akimkaribisha Bradley kwa furaha na hata kupanda juu ya kiti ili aweze kutoshana na yeye.