“Mimi ni baby girl, siwezi chumbiana na wanawake,” Kinuthia

Baadhi walitafsiri kwamba Kinuthia amekiri kuwa anatoka kimapenzi na wanaume, licha ya kuwa anajulikana kama mwanaume anayevaa mavazi ya kike tu.

Muhtasari

• Kupitia Instagram, Kinuthia alichapisha video wakiwa wanatembea pamoja na Shiphira na kuiambatanisha na mada ‘samahani, sisi si wasagaji’.

• “Hehehehe mimi mniache, mimi ni mtoto wa kike hivyo siwezi toka kimapenzi na wanawake,” Kinuthia aliandika akimteg Shiphira.

Kinuthia
Kinuthia
Image: Facebook

Crossdresser Kelvin Kinuthia ametoa maelezo kuhusu uhusiano wake wa karibu na rafiki yake, Shiphira.

Hii ni baada ya baadhi ya watu mitandaoni kuibua tetesi za kutaka kufahamu kwa kina iwapo Kinuthia na Shiphira wana uhusiano wa kimapenziv au ni urafiki tu.

Kupitia Instagram, Kinuthia alichapisha video wakiwa wanatembea pamoja na Shiphira na kuiambatanisha na mada ‘samahani, sisi si wasagaji’.

Aliongeza akisema kwamba si mara moja yeye ameweka wazi kwamba ni mtoto wa kike, hivyo hakuna uwezekano wa aina yoyotev kwamba anaweza toka kimapenzi na wanawake.

“Hehehehe mimi mniache, mimi ni mtoto wa kike hivyo siwezi toka kimapenzi na wanawake,” Kinuthia aliandika akimteg Shiphira.

Hata hivyo, kauli hii ilionekana kuwachanganya wengi ambao kwa njia ya moja kwa moja walitafsiri kwamba Kinuthia amekiri kuwa anatoka kimapenzi na wanaume, licha ya kuwa anajulikana kama mwanaume anayevaa mavazi ya kike tu.

Hii si mara ya kwanza kwa Kinuthia kudokeza kuwa yeye angependelea kuitwa ‘babygial’ akisema kwamba huwa anaudhika pindi anapokutana na mtu mtaani na kumuita ‘kaka’.

“Hapana, hapana, hapana rafiki zangu, mimi kuna kitu kimenikasirisha. Yaani tunakutana na wewe kwa Mall ama tuseme kwa Supermarket. Na huu urembo wote, na hizi kucha zote, unaniambia ‘niaje bro?’… kwanza tuanzie hapo, kaka yako ni nani?” Kinuthia aliuliza.

 “Ama mtu unanikujia na salamu za kugongana hapa kwa mabega, aaaagh na ukinivunja mabega? Mimi kama huwezi nisalimia na mkono ama huwezi nipa hug, salamu zako ukae nazo. Na kama unajua utaniambia ‘niaje bro’ sitaki. Kama huwezi niita ‘baby girl’  tafadhali kaa na salamu zako,” aliongeza.