“Wakati mgumu kabisa maishani ni nilipogundua binti yangu hayuko hai” - Willis Raburu

Raburu alifichua kwamba wakati huo ilimbidi kurejelea uhusiano wake na Mungu na hata kwa wakati mrefu ilimbidi achukuev likizo mbali na Mungu.

Muhtasari

• Hata hivyo, alifichuac kwamba kwa sasa uhusiano wake na Mungu umerudi kama ulivyokuwa zamani.

• Wakati ip huo, ndio masuala mengi yaliibuka katika ndoa yake kupelekea kusambaratika.

WILLIS RABURU,
WILLIS RABURU,
Image: hisani

Mtangazaji Willis Raburu amefunguka kuhusu wakati mgumu zaidi aliopitia katika maisha yake.

Akizu8ngumza kwenye podikasti ya Lessons @30 na Dr Ofweneke, Raburu alifichua kwamba wakati aligundua bintiye hangeweza kuishi pindi tu baada ya kuzaliwa, alijihisi mnyonge kupita kiasi na kipindi hicho kilikuwa kigumu sana kwake.

“Wakatio mgumu kabisa kwangu ni wakati niligundua kwamba binti yangu asingeweza kuishi tena. Wakati binti yangu aqlikufa, hicho ndicho kilikuwa kipindi kigumu zaidi kwangu. Sidhani kuna uchungu mwingine ambao unaweza kulinganishwa na huo,” Raburu alisema baina ya miguno ya hisia za uchungu.

Alieleza kwamba alitaarifiwa kuhusu kifo cha mwanawe akiwa hospitalini na ilikuwa ni mwisho wa mwaka wakati watu wengine walikuwa wanashetrehekea kukaribisha mwaka mwingine.

“Ulikuwa ni wakati mweusi sana kwangu, nilikuwa bado pale hospitalini. Hata niko na tattoo hapa katika mkono wangu, ilikuwa ni Desemba 31 wakati watu wanangoja mwaka mpya,.”

“Kila kitu kilikuwa sawa, tulienda kwa daktariv kila kitu kilikuwa tu sawa, halafu ghafla tunaambiwa kwamba mapigo ya moyo wa mtoto hayapigi. Sifikirii kuna wakati nimewahi hisi kuwa mpweke gizani na uchungu kama wakati ule,” aliongeza.

Raburu alifichua kwamba wakati huo ilimbidi kurejelea uhusiano wake na Mungu na hata kwa wakati mrefu ilimbidi achukuev likizo mbali na Mungu.

Hata hivyo, alifichuac kwamba kwa sasa uhusiano wake na Mungu umerudi kama ulivyokuwa zamani.

Wakati ip huo, ndio masuala mengi yaliibuka katika ndoa yake kupelekea kusambaratika.

Raburu na aliyekuwa mpenziwe, Marya Prude walipoteza mwanao mwishoni mwa 2019 na kwa wakati mmoja Marya akakiri kwamba haamini katika uwepo wa Mungu tena.