•Rapa Stevo Simple Boy arejea mara tena na mtindo mpya wa nywele ,raondi hii ikiwa ni zamu yakuwa 'rastaman',jambo ambalo limewasisimua mashabiki katika mitandao ya kijamii kutokana na video hiyo ambayo inamwonesha 'mzee wa mitulinga' akiwa na rasta.
Msanii Stevo Simple Boy ,almaarufu mzee wa mitulinga, tena kaja na mtindo mpya wa rastaman raundii hii akijjiita Lucky Dube.
Aidha ,baadhi ya mashabiki wake wameonekana kutofurahiswa na mtindo huo ,"stevo anatuambia kupumzika ni mbinguni" mmoja wa mashabiki alisema.
Kutokana na video iliyosambazwa mitandaoni na kinyozi mmoja maarufu humu nchni,Simple Boy,sasa ameweka rasta akiiga aliyekuwa muimbaji wa reggea,Lucky Dube.
Ni majuzi tu alipotengeneza nywele zake na kuwekwa ndevu bandia na mashabiki kumfananisha na muimbaji Rick Ross.
Hili linakuja siku chache baada ya msanii huyo kusema kwamba atamlipisha msanii kutoka Tanzania Diamond Platinumz shilingi 20M ,ili wafanye colabo.
Vile vile ,mashabiki katika mitandao ya kijamii wamesema kuwa Stevo ni msanii ambaye upenda mambo mapya na wanamkubali kabisa na ambapo kwa kipindi cha takriban mwezi mmoja amekuwa akionyesha mtindo mpya wa mavazi na mwonekano.
Muimbaji huyo aliyeimba kibao kama vile 'mihadarati', amekuwa akiwachangamsha mashabiki wake na misemo mipya ya ucheshi na vile vile mavazi mapya kila mara.