Marioo aingia kwenye ligi kubwa, amtambulisha msanii wa kwanza kwenye lebo yake

Kufuatia utambulisho huo, Marioo sasa anaingia kwenye ligi za kibabe na wasanii kama Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Nandy, Alikiba miongoni mwa wengine wanaomiliki rekodi lebo na wasanii.

Muhtasari

• Hatimaye, ngoja ngoja hizo zilifika ukingoni siku ya Alhamisi alipomtambulisha msanii chipukizi kwa jina Stans Ooh kama kifungua mimba katika lebo yake mpya kwa jina Bad Nation.

marioo amsaioni stans ooh
marioo amsaioni stans ooh

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo amemtambulisha msanii wa kwanza katika lebo yake ya Badnation.

Marioo kwa siku kadhaa zilizopita amekuwa akidokeza kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuhusu ujio wa msanii wakem pya.

Hatimaye, ngoja ngoja hizo zilifika ukingoni siku ya Alhamisi alipomtambulisha msanii chipukizi kwa jina Stans Ooh kama kifungua mimba katika lebo yake mpya kwa jina Bad Nation.

Kufuatia utambulisho huo, Marioo sasa anaingia kwenye ligi za kibabe na wasanii kama Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Nandy, Alikiba miongoni mwa wengine wanaomiliki rekodi lebo na wasanii.

Katika kundi la kizazi kipya, Diamond aliwafungulia njia wenzake mwaka 2016 alipozindua Wasafi, akafuatiwa na Alikiba na Kings Music.

Baada ya kujiondoa WCB Wasafi mwishoni mwa 2019, Harmonize aliondoka na kuanzisha lebo yake ya Konde Music Worldwide na kusaini kadhaa wakiwemo Anjella na Ibrah naye Rayvanny akaanzisaha yake Next Level Music mwaka 2022 akimsaini Macvoice.

Aidha, Nandy naye alianzisha lebo yake ya African Princes ambayo alisema ni mahususi kwa wasanii wa kike pekee na kumsaini Yammi.