• Kuondoka kwa Nyagwoka kunajiri wiki mbili tu baada ya mtangazaji mwenzake katika kituo hicho, Esther Mwende Macharia kutangaza kuondoka baada ya cmiaka 14.
Msomaji wa habari katika stesheni ya Radio Maisha, Mike Nyagwoka amethibitisha kuondoka katika kituo hicho kinachimilikiwa na shirika la habari la Standard.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Nyagwoka alisimulia jinsi alijitahidi kubadilisha kasumba na kuvuta mafanikio makubwa kwa jina lake.
Alifichua kwamba aliondoka Radio Maisha takribani mwezi mmoja uliopita lakini wakati huu ndio mwafaka kufichua kwa mashabiki wake kuwa ameaga stesheni hiyo.
“Nilipoondoka kuelekea nyumbani baada ya kazi tarehe 31 Julai 2024, hakukuwa na dalili zozote kwamba nilikuwa nimefanya ziara yangu ya mwisho mahali hapa. Ingekuwa chaguo langu ningeshikilia kwa muda mrefu kidogo lakini kete zilikuwa zimepigwa na maamuzi yalifanywa na nilichopaswa kufanya ni kutii,” Nyagwoka alisema.
“Radio Maisha ilikuwa safari nzuri ambapo nilionyesha kwamba mtu anaweza kushinda dhiki na kubaki kwenye njia ya ndoto yake. Ninajivunia chapa niliyounda na kazi niliyofanya. Dhamira yangu ilikuwa kuacha urithi na ninaamini nilifanya.”
“Tunaishi katika enzi ambayo inatoa fursa nyingi na ni matumaini yangu kuwa nitapata motisha sahihi ya kuzitumia ili kujiweka sawa. Ninaomba vile vile kwamba milango mingine itafunguliwa hivi karibuni,” aliongeza.
Kuondoka kwa Nyagwoka kunajiri wiki mbili tu baada ya mtangazaji mwenzake katika kituo hicho, Esther Mwende Macharia kutangaza kuondoka baada ya cmiaka 14.