Stevo Simple Boy avunja kimya baada ya kupoteza akaunti yake ya TikTok

Stevo si kwa kwanza kupatwa na pigo hilo kwani wenzake kama Mulamwah, Baba Talisha na wengine waliwahi fungiwa akaqunti za TikTok.

Muhtasari

•   “Akaunti yangu ya tiktok imebaniwa, naomba unanifollow kwenye akaunti yangu mpya, stevo simple official, asante tafadhali mashabiki wangu na Mungu awabariki,” Stevo alitaarifu.

Msanii Stevo Simple Boy amevunja kimya chake baada ya kupoteza akaunti yake ya TikTok.

Stevo Simple Boy aliweka wazi kwamba akaunti yake ya TikTok iliyokuwa na wafuasi zaidi ya 348k ilifungwa na mamlaka ya mtandao huo kwa njia tatanishi.

Akionekana kuwa mwenye mawazo mengi, msanii huyo aliwataarifu wafuasi wake kwamba ameanzisha chaneli nyingine na kuwataka mashabiki hao kuendelea kumfuata kwa ajili ya maudhui zaidi ya muziki na ucheshi wake.

“Akaunti yangu ya tiktok imebaniwa, naomba unanifollow kwenye akaunti yangu mpya, stevo simple official, asante tafadhali mashabiki wangu na Mungu awabariki,” Stevo alitaarifu.

Aidha, katika klipu hiyo fupi, msani huyo ambaye katika siku za hiviu karibuni amekuwa akiwakosha wafuasi wake kwa fasheni za kipekee kutoka kwa mtindo wa nywele na uvaaji, alisema kwamba hata yeye mwenyewe haelewi kilichosibu akaunti ya awali.

“Manze nimefungua tiktok mpya kwa sababu ile yta kitambo imepigwa marufuku, hivyo tafadhali naomba mnifollow kwa hii akaunti mpya na mambo yatakuwa mwake mwake, ama vipi?” aliongeza.