Dr Ofweneke atema moto wa hasira kisa kuitwa ‘Local YouTuber’ na runinga moja humu nchini

Alivitaka vyombo vyote vya habari nchini kuwapa maua yao watu maarufu jinsi inavyostahili pindi wanapoamua kutumia maudhui yao katika stori zao, akisema ‘hautakufa na hautanuka’.

Muhtasari

• Alivitaka vyombo vyote vya habari nchini kuwapa maua yao watu maarufu jinsi inavyostahili pindi wanapoamua kutumia maudhui yao katika stori zao, akisema ‘hautakufa na hautanuka’.

DR OFWENEKE.
DR OFWENEKE.
Image: HISANI

Mchekeshaji na muundaji wa maudhui Dr Ofweneke ameonyesha kukasirishwa kwake na tovuti ya kituo kimoa cha runinga cha hmu nchini kumtambua kama mtengenezaji wa maudhui ya YouTube nwa humu nchini.

Ofweneke alichukua kwenye Instagram yake kuonyesha ghadhabu yake akisema kwamba hawakumtambulisha jinsi anastahili kutambulika baada ya kuandika Makala yao kutoka kwa mahojiano ya Ofweneke na mgeni wake katika podikasti yake ya YouTube, Lessons At30.

Alivitaka vyombo vyote vya habari nchini kuwapa maua yao watu maarufu jinsi inavyostahili pindi wanapoamua kutumia maudhui yao katika stori zao, akisema ‘hautakufa na hautanuka’.

“Mnaona aibu gani katika kutaja Lessons At30 na Dr Ofweneke. Mimi naitwa Eagle mwenyewe, Duke wa Kakamega Dr Ofweneke, na sio Local YouTuber. Jifunze kuwapa maua "youtubers" wote na watungaji maudhui pindi unapochukua hadithi zao, hautakufa na hautanuka,” Ofweneke alisema.

Wanablogi mbalimbali na wakuza maudhui walifurika katika chapisho hilo wakimtetea Ofweneke na kudai kuwa vi vyema watambuliwe jinsi inafaa pindi mtu anapoamua kutumia maudhui yao kuchapisha Makala kwenye tovuti yake.

Maoni yako ni yepi?