• “Hii kitu [ya kurap] bado iko, tunarudi kule kwa ajili ya kizazi hiki kwa sababu hawawezi kua wakianguka nayo, tutainuka nao." aslisema.
Mchungaji wa kanisa la Life Church International lililoko maeneo ya Limuru kaunti ya Kiambu, Pastor T Mwangi ametangaza kwamba yuko tayari kurudi katika kuimba miziki ya kufoka ya injili kwa ajili ya kukomboa kizazi cha sasa.
Akizungumza katika kongamano kuu la injili la Rhema Feast lililofanyika katika uwanja wa Kasarani, mchungaji huyo alisema kwamba yuko tayari kufanya chochote katika uwezo wake kama pasta kuhakikisha anakirejesha kizazi cha sasa kanisani.
Mchungaji huyo alionyesha uhodari wake katika kutema mistari kwa njia ya kufoka na kukiri kwamba suti anavaa tu kwa sababu ya uchungaji lakini akiamua ana uwezo wa kurudi katika ku’rap miziki ya injili na kuwarudisha vijana kanisani.
“Hii kitu [ya kurap] bado iko, tunarudi kule kwa ajili ya kizazi hiki kwa sababu hawawezi kua wakianguka nayo, tutainuka nao. Hii suti isiwadanganye, hii navaa tu juu ya askofu lakini tukiamua kurudi evangelism tutarudi na ubaya. Tutawapigia rap, tutawahubiria, na tutawapaka mafuta ya upako. Juu kinakaa kimeumana ni mbaya-mbaya, kizazi hiki hakitakufa bila injili. Kama ni kupiga mashoo tutapiga hadi tuhakikishe kizazi kinasikiliza injili katika wakati wetu,” Pastor T Mwangi alisema huku umati ukimshangilia.
Tazama video hiyo akirap hapa;