• Marco Joseph alizikwa Jumapili iliyopita, siku mbili baada ya kifo chake katika hospitalini moja nchini Tanzania alikokuwa anatibiwa.
Kikundi cha wanamuziki wa injili kutoka Tanzania, Zabron Singers wametunga wimbo mpya kumuomboleza na kumpa buriani mwenzao aliyefariki wiki jana, Marco Joseph.
Katika wimbo huo huo wenye mada ‘Inaniuma Sana’ wanakwaya hao walionekiana wenye huzuni mwingi wakiwa wamevalia mavazi meusi ishara ya kuomboleza.
“Hili limeniliza sana, hili limeniumiza sana, awamu hii nimeumia sana, Mungu wangu nisaidie. Mboona umeniacha sana, katika hili nimeumia sana, nakiri nakuhitaji sana, Mungu wangu nisaidie….”
“Ungeniuliza singekubali mimi mpendwa wangu nimuache aende, rafiki yangu kipenzi aende, Mungu hapana, kwangu si sawa. Ile mipango tulipanga imezima, kwako ni sawa ila nabaki peke yangu, nitafanyaje nimebaki peke yangu, Mungu hapana kwangu si sawa…” sehemu ya wimbo huo unaimba kwenye aya za utangulizi.
Marco Joseph alizikwa Jumapili iliyopita, siku mbili baada ya kifo chake katika hospitalini moja nchini Tanzania alikokuwa anatibiwa.
Alikuwa mwimbaji mkuu wa kwaya maarufu ya Tanzania mwimbaji Zabron ambayo inajumuisha Japhet Zabron, Victoria Zabron, Jamila Dotto, Samuel Joseph, Semroza Godfrey, Grace Madata, na Joyce Zabron.
Waimbaji wa Zabron waliibuka kidedea kupitia wimbo wao wa 'Mkono Wa Bwana’ wimbo ambao mwalimu wao, Japhet Zabron alisema ndio mpaka leo hii unawatambulisha kila mahali wanapokwenda.